MPANGO WA KUHIFADHI MBEGU ZA KIUME KATIKA UMRI WA MIAKA 18

MBEGU za uzazi wa wanaume zinapaswa kuvunwa na kuhifadhiwa pindi mtu anapotimiza umri wa miaka 18.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtafiti wa masuala ya uzazi nchini Uingereza, manii ya mwanaume huwa katika hali bora zaidi wakati huo na hivyo yainapaswa kuvunwa na kisha kutumika kupandikiza wanawake katika siku za usoni.
Daktari Kevin Smith, ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Abertay kilichoko Dundee, Uingereza, anasema kuwa baada ya utafiti wa kipindi kirefu amebaini kuwa ni bora kuvuna manii mapema ili kuepuka maradhi mengi yanayochangiwa na kuongezeka kwa umri.
Dakta Kevin Smith, anasema kuwa Wizara ya Afya ya Uingereza inapaswa kuunda hifadhi maalum ya mbegu za uzazi
Daktari Kevin Smith ameorodhesha ugonjwa wa akili ”autism”, na ule wa kuchanganyikiwa ama ”schizophrenia” miongoni mwa magonjwa mengine mengi.
Dakta Smith, anasema kuwa wizara hiyo inapaswa kuunda hifadhi maalum ya mbegu za uzazi ili kupunguza matukio ya mtu kukumbwa na maradhi aliyoyaorodhesha.
Maoni yake, hata hivyo, yanapingwa na muungano wa wauguzi wa uzazi ambao wanasema kuwa hilo halitakuwa suluhisho la kudumu.
Badala yake shirika hilo linaitaka serikali ya Uingereza iweke sera zitakazowasaidia Waingereza waliofikia umri wa uzazi kupata ajira.
Takwimu zinaonesha kuwa wanaume wanaanza kupata watoto wakiwa na umri wa miaka 33, hilo likiwa ni ongezeko kutoka kwa miaka 31 katika miaka ya tisini.
Akitetea wazo lake katika jarida la madaktari la ”The Journal of Medical Ethics, Dk. Smith anasema kuwa wale wanaotaka kupata watoto mapema basi wafanye hivyo lakini kwa wale ambao wamefikisha miaka 40 ni vyema watumie mbegu walizohifadhi kwa matokeo mazuri zaidi.
Profesa Adam Balen, wa shirika la British Fertility Society, ameonya kuwa mbegu zilizohifadhiwa huwa hazina nguvu kama zile zinazotolewa moja kwa moja.
Amebaini kuwa ni bora kuvuna manii mapema ili kuepuka maradhi mengi yanayochangiwa na kuongezeka kwa umri.
Wakati huohuo, mwanasayansi Sheena Lewis aliwashauri wanaume waanze kushughulikia suala la familia mapema katika ujana wao.
”Ninataka kuwaambia kuwa umri mzuri wa kuzaa kwa wanaume na wanawake ni kati ya miaka ya 20 na 30.”

Comments