James Mbatia: Mjue kwamba, kwenye UKAWA, Kahangwa alikuwa mgombea ambae ametia nia kwa NCCR mageuzi, Lipumba likuwa ametia nia kwa chama chake cha wananchi CUF na CHADEMA wakasema sisi kwenye kamati kuu tumeshavuka hatua zote, mgombea wetu Dr. Slaa, nikiwa nae high table pale millenium tower na Dr. Kahangwa akasema naomba wagombea wenzangu watatu tukutane tuzungumze ili tupate suluhisho la kumpata mmoja, ndio wakaenda kukutana nyumbani kwa professa LIpumba. Dr Slaa, Prof. Lipumba na Dr. Kahangwa tarehe 12/07/2015 siku ya Jumapili. Wakazungumza wagombea wote watatu, kila mtu akaeleza vigezo vyake, na kwanini walienda wakakaa wakazungumza?
Tulipata mtafaruku mkubwa tarehe 17/06/2015. Nilitika bungeni Dodoma kwa ajili ya mkutano huo, ilikuwa siku ya Jumatano, Serena Hotel, tuko Maalim Seif, Dr. Slaa, Prof Lipumba, Freeman Mbowe, James Mbatia, Emmanuel Makaidi na katibu mkuu wa NLD na Dr Kahangwa.
Dr. Slaa akasema mimi ndie bora kuliko wengine, akawa anaulilia Urais kwa nguvu kubwa, tuwe wakweli tu, biblia takatifu St. John anatuambia ukweli utatuweka huru, sura ya 8:32, karibu kikao kivunjike saa nane za usiku kwa kutokuelewana ndio maana Dr. Kahangwa akaja kuomba tukutane na akaja na points zake 15.
Tarehe14/07/2015 siku ya Jumanne Colisium hotel waandishi wa habari mlikuwa mnasubiri tangu asubuhi, saa tatu za usiku mimi ndio nilikuwa mwenyekiti wa kile kikao, tukiwa na Dr. Slaa, Mbowe na wenzake. Siku hio ndio tulikuwa tunatakiwa tutangaze mgombea Urais, mimi ndio nikatamka, naombeni mtupe siku saba tu tutamtamka na kwanini! Mheshimiwa Mbowe aliomba tuwaachie chama chao wafanye hivyo na Dr. Slaa aliomba naomba msinitangaze leo, ngoja tukafanye utaratibu wa mbwembwe na taratibu za kunitangaza. Leohii anasema hajawahi kutia nia wala shamsham za kugombea Urais, anasema siasa ni sayansi, yeye anaamini kwenye usafi.
Nilikuwa nimtangaze tarehe 14 wakati huo Lowassa hajaingia CHADEMA. Aliyeenda hadhari kumtaka Lowassa ajiunge na UKAWA kwenye ofisi za CUF tarehe 27/7/2015 alikuwa James Mbatia, aliehariri ile statement yote, namheshimu sana na mpaka kesho ni rafiki yangu kwelikweli, alikuwa Prof Lipumba.
Dr Slaa yeye anasema kwamba yeye saa tatu za usiku tarehe 28 ndio aliamua kutoka ndani ya CHADEMA kwa sababu tarehe hio kamati kuu inamsikiliza Edward Lowassa wakati sio mwanachama wa CHADEMA, mnaokumbuka tarehe 28 siku ya Jumanne tulikutana bahari beach saa tatu usiku za siku hiyo, saa tisa alasiri Edward Lowassa alikuwa mwanachama wa CHADEMA tayari, rejeeni kumbukumbu zenu.
Mimi niombe tu watanzania hizi hoja nyepesi za kutaka kulipasua taifa la Tanzania badala ya kujadili hoja za msingi za kuleta muafaka wa kitaifa, kuwaunganisha watanzania pamoja, kuleta maridhiano ya kitaifa na watanzania naomba walewe UKAWA maana yake nini. UKAWA tunasimamia uhai wa taifa la Tanzania, utu wa mtanzania, uzalendo wa taifa, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji, tunawataka watanzania wote tuje pamoja, tuwe kitu kimoja na hii itawezekana kutokana na sauti ya watanzania iliyopo ndani ya rasimu ya pili ya tume ya mabadiliko ya katiba ili tuwe na katiba ili yoyote atakaekuwa pale aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Niwaombe watanzania kwa nia njema, kila mtu ana haki ya kutoa mawazo yake, kila mtu ana haki ya kutoa fikra zake lakini wanasiasa na hasa wale wa CCM, wengine wanasema twende kwenye midahalo, nakubali twende kwenye midahalo. Nawakaribisha kwenye mdahalo na mimi, wala wasimsumbue Rais wala sio saizi yao, nawakaribisha sio saizi yao, waje kwenye mdahalo na mimi.
Mzee Sitta anaeomba mdahalo nitamuuliza, alijenga ofisi ya spika Urambo akiwa madarakani kwa milioni 500, Je kuna ofisi ya spika Urambo? Matibabu ya zaidi ya milioni 200 aliyoyafanya akiwa spika wakati ananunua dawa kwenye pharmacy na rekodi zote tunazo, Je milioni 200 zinanunua dawa baridi? Makochi ya ofisi ya spika? Juzi Sitta ametuambia kuhusu vichwa vya treni feki ndio sababu nawaambia hakuna atakaepona hapa waache hizi cheap politics. Nawaheshimu tu ni wazee wangu. Tangu 1988 yeye alikuwa rafiki yangu, Magufuli tangu chuo kikuu yeye akiwa mbele yangu, kati ya watu walionichangia harusi yangu ni pamoja na Dr. Magufuli nikiwa na mchumba wangu mwaka 98, hivi kweli tukisimamiai leo hii tukimwambia aeleze jinsi alivyosimamia uuzwaji wa nyumba za serikali na kashfa ya uuzaji wa nyumba za serikali, atapona?.
Hivi ni viashiria kwamba CCM sasa imeshindwa hoja, wanaleta mambo ya udini, mara maaskofu wamepewa rushwa, mara masheikh wamefanya hivi, mara kashfa kwa masheikh, mara wanahusisha masheikh na ugaidi. Nawaomba chama cha mapinduzi, sote sisi ni watanzania, Namuomba amiri jeshi mkuu Jakaya Kikwete, rafiki yangu na kaka yangu, 2013 ilivyoibuka hoja kuchinja ni ibada au sio ibada, mauaji yaliyotokea Zanzibar ya mapadri mwezi wa pili, mauaji yaliyotokea Shinyanga kwa wachungaji, masheikh wanamwagiwa tindikali Zanzibar, hali ya sintofahamu Tanzania ikawa ni tense. Balozi wa Vatikan anapigwa bomu kule Arusha. Ilibidi turudi kama taifa tukae, tulikuwa hatufiki zaidi ya watu 100 tukakaa kutafakari taifa linakwenda wapi. Baada ya pale kutoka kitu kimoja, hakuna mauaji ya padri yaliyotokea, hakuna kumwagiana tindikali halafu hapa wanasema ni magaidi wanafanya vitu hivi, mbona tulikaa sisi tunaojiita wakubwa hatukufika 100, hakuna mauaji.
Niwaombe watanzania ambao ni zaidi ya milioni 46, wasiruhusu watu ambao hawazidi mia moja walipasue taifa la Tanzania na tujue Tanzania ni yetu sote.
Viongozi wa dini wasiwajibu watu hawa, watanzania wafanye maamuzi sahihi kwenye sanduku la kura ili Jakaya Kikwete akabidhi nchi kwa amani. N a minong'ong'ono CCM haitakabidhi madaraka, dhana ya jeshi kuchukua madaraka sio jeshi ninalolijua lililoasisiwa na Mwalimu Nyerere. Dhana ya jeshi litachukua madaraka imepitwa na wakati.
Mwisho wale wanaotishia kuchukua madaraka, tuwaambie Kenya mwaka 2012 walitishia sana Kenyatta ana kesi the hegue na wakenya wakamchagua. Siasa nyepesi, hawa wanaosimamia vyombo vya ulinzi na usalama washaurini vizuri hawa watawala wachache wasianze kuhema hema na vijana walio wengi tusiruhusu watu wachache walio madarakani eti kwa lolote lile wabaki madarakani. Tanzania bila CCM yawezekana.
Tuwe wakweli eti unasema unapewa rushwa ya milioni mia tano 2008 huripoti popote, unakuja kuisema leo baada miaka saba!, hivi inaingia akilini! Unajua kusema uongo ni shida sana, afadhali useme ukweli utakuwa unakumbuka, niwaombe watanzania tuwe makini sana na watu hawa, James nisipokuwa Rais isiwe nongwa kwa kulifarakanisha taifa la Tanzania, isiwe nongwa na wale wote wanaojaribu kuleta machafuko ya aina yoyote, the hague ipo, zimebaki siku hamsini, hawawezi kurudisha moyo wa watanzania nyuma, sisi mgomvi wetu ni CCM, lazima iondoke.
Asanteni kwa kunisikiliza, mwenyezi Mungu awabariki sana.
=======
=======
MASWALI
Katika maelezo yako, umesema kwa yaliyotokea jana, umesema CCM inaashiria kushindwa, wa jana kasema yeye hana chama. Kwanini umezungumzia CCM inaelekea kushindwa ilhali aliesema hana chama?Kuna ukweli gani kwamba Slaa na nyie mlishirikiana Lowassa kugombea urais?(Jamboleo)Umezungumzia maswala ya dini, kwanini unawazungumzia viongozi wa dini ambao wenyewe hawajajititokeza kujibuRICHMOND ni tukio la kupangwa au ni kweli?!(Radio1)Kutokana na hali ya halisi, msimamo wenu ukoje?(TBC 1)Naomba ufafanuzi, baada ya kusikia maelezo yote kutoka kwa aliekuwa naibu katibu mkuu wa CHADEMA, amezungumzia kashfa moja tu ya Richmond na kuacha zote, nyinyi mmelipokeaje, nyuma yake kuna nini?(Nipashe)
Katika maelezo yako, umesema kwa yaliyotokea jana, umesema CCM inaashiria kushindwa, wa jana kasema yeye hana chama. Kwanini umezungumzia CCM inaelekea kushindwa ilhali aliesema hana chama?Kuna ukweli gani kwamba Slaa na nyie mlishirikiana Lowassa kugombea urais?(Jamboleo)Umezungumzia maswala ya dini, kwanini unawazungumzia viongozi wa dini ambao wenyewe hawajajititokeza kujibuRICHMOND ni tukio la kupangwa au ni kweli?!(Radio1)Kutokana na hali ya halisi, msimamo wenu ukoje?(TBC 1)Naomba ufafanuzi, baada ya kusikia maelezo yote kutoka kwa aliekuwa naibu katibu mkuu wa CHADEMA, amezungumzia kashfa moja tu ya Richmond na kuacha zote, nyinyi mmelipokeaje, nyuma yake kuna nini?(Nipashe)
Majibu
Kwamba Slaa hana chama, tunamuhusishaje na kushindwa kwa CCM. Alisema yeye mwenyewe, siku zote tunajadili hoja sio wote lakini ukimsikiliza.., kati ya vyombo vya habari, chombo gani jana cha habari kilirudia? Sawa wamelipa, wamefanya nini, sisi hatuna matatizo. Demokrasia inasema siku zote wengi wape, tarehe 20/07 tukiwa na Lipumba, Lowassa, Mbowe na wengine wote. Lowassa hajawahi kutamka atakuja na wabunge 50 hajawahi kutamka. Alisema walivyokuwa CCM walikuwa wanamshabikia, alieyasemea wapi!. Hata angesema angekuja nao, bila Lowassa wale watu wa Jangwani wangetoka wapi.
Kwamba Slaa hana chama, tunamuhusishaje na kushindwa kwa CCM. Alisema yeye mwenyewe, siku zote tunajadili hoja sio wote lakini ukimsikiliza.., kati ya vyombo vya habari, chombo gani jana cha habari kilirudia? Sawa wamelipa, wamefanya nini, sisi hatuna matatizo. Demokrasia inasema siku zote wengi wape, tarehe 20/07 tukiwa na Lipumba, Lowassa, Mbowe na wengine wote. Lowassa hajawahi kutamka atakuja na wabunge 50 hajawahi kutamka. Alisema walivyokuwa CCM walikuwa wanamshabikia, alieyasemea wapi!. Hata angesema angekuja nao, bila Lowassa wale watu wa Jangwani wangetoka wapi.
Watanzania wameshamchagua tayari Lowassa, hata picha za bahari beach zinaonyesha Slaa alikuwa pembeni anazungumza na Lowassa. Tuliwashawishi waje, watanzania walikuwa na hofu hawa hawana uzoefu. Wana uzoefu, aliemteua Lowassa waziri mkuu wa kwanza alikuwa Kikwete, machafuko yalitokea wapi? Slaa alikatwa ubunge CCM akaja CHADEMA, hakupewa masharti yoyote, katiba ndio inaweka taratiba, wewe unajifanya unaweka masharti juu ya taratibu, kama alikuwa na masharti yake hio ni fujo.
Sikuwahi kukutana na baba askofu Gwajima kwenye mchakato, kama kuna mtu alimtuma Gwajima nani alimtuma, hata kwenye picha Gwajima alipokuwa hospitali aliekuwa karibu yake ni Slaa. Hakuna mtu ambae hakuwa juu ya sheria.
Viongozi wa dini
Hivi maaskofu waje wajitetee kuwa wamekula rushwa au hawajala!, naomba wasijibu. Tutaleta mifarakano, tunaomba TEC ikiwapendeza wanaweza wakatoa statement moja tu.
Hivi maaskofu waje wajitetee kuwa wamekula rushwa au hawajala!, naomba wasijibu. Tutaleta mifarakano, tunaomba TEC ikiwapendeza wanaweza wakatoa statement moja tu.
Richmond
Nimesoma barua ya ufisadi, ufisadi ni mfumo na Lowassa wana haki ya kujielezea zaidi wakitaka lakini hawa wanataka kututoa kwenye reli tuanze kujibizana mmoja na wengine.
===
Nimesoma barua ya ufisadi, ufisadi ni mfumo na Lowassa wana haki ya kujielezea zaidi wakitaka lakini hawa wanataka kututoa kwenye reli tuanze kujibizana mmoja na wengine.
===
Ametoa msimamo wake ndani ya chama chake na maswala haya yanatakiwa yamaliziwe ndani ya chama chake, swala la professa Lipumba na swala la Dr. Slaa ni vitu tofauti kabisa. Professa Lipumba alikuwa anazungumzia maswali ya principles na maswala alisema yanamsuta yeye lakini kwa kiasi flani labda..
Maswala ya Dr. Slaa ya jana ni masuala ya kulipasua taifa la Tanzania, maswala ya Dr Slaa ya kusema hakuwahi kuteuliwa, haya ni masuala ndani ya chama chake na majibu niliyosikiliza hata BBC jana Lissu akimjibu tuhuma hizo ndani ya CHADEMA. Kwanini nimezungumza hapa, NCCR mageuzi mgombea wetu ndani ya UKAWA ni Lowassa, tuna haki ya kuyasema hayo, UKAWA ni umoja wa watanzania wote, kilichotusikitisha jana ni kuhusishani na watu wengine, ugomvi unapanuka sasa, unatoka kwenye vyama vya siasa unalipasua taifa la Tanzania, tunasema hapana. Wacha vyama vya siasa sisi tusuguane, migongano ya kifikra ikichukuliwa chanya inaweza kuleta uhai zaidi kwa taifa la Tanzania.
Yaliyotokea jana naamini ni chanya na yameliimarisha zaidi taifa la Tanzania, watanzania wanasema tusirudi nyuma, msimamo ni ule ule, umetuimarisha zaidi. Tuchukulie mfano mkutano wa tarehe 29, hivi unaweza ukaja mbele ukasema tulibeba watu kwa mabasi! Ni siasa ambazo nimesema ni za mitaroni, sisi tujadili hoja, tusimjadili Dr. Slaa.
Chanzo jf
Chanzo jf
Comments
Post a Comment