Msanii maarufu zaidi duniani kwenye mtandao wa Instagram Taylor Swift ameshtakiwa kwa kuiba mistari ya wimbo wake maarufu Shake It Off.
Iwapo atapatikana na hati mwanamuziki huyo anakabiliwa na faini ya dola milioni 42.
Mwanamuziki mwenza Jesse Braham vilevile raia wa marekani amedai kupitia kwa wakili wake kuwa Swift aliiba mistari ya wimbo wake alioutunga mwaka wa 2013 unaoitwa 'Haters Gone Hate'.
Mbali na kufidiwa pesa hizo Braham, anataka jina lake lijumuishwe katika rekodi za wimbo huo kama aliyechangia utunzi wake.
Mawakili wa Swift hawajajibu madai ya kesi hiyo inayomkabili.
Kibwagizo cha wimbo wa Braham ni : "Haters gone hater, playas gone play/ Watch out for them fakers, they'll fake you everyday."
Kibwagizo cha wimbo wa Taylor Swift ni : "Cause the players gonna play, play, play, play, play/ And the haters gonna hate, hate, hate, hate, hate."
Katika mstari mwengine Swift anaimba : "And the fakers gonna fake, fake, fake, fake, fake."
Kwa mujibu wa mchunguzi wa muziki ,japo maneno hayo yanafanana kimuziki utunzi wa swift haufanani hata kidogo na ule anaodai Brahama.
Braham anasema kuwa amechukua hatua hiyo ya kwenda mahakamani baada ya kujaribu bila mafanikio kutafuta ridhaa kutoka kwa kampuni inayorekodi Swif , Big Machine.
''Nimekwenda kwao mara tatu nne ama hata tano hivi kuwashauri kuhusiana na jambo hilo lakini wamenipuuza.'' alisema Braham.
Awali anadaiwa kuwa alitaka kupigwa selfi na Swift mbali na kutajwa kama mmoja wa watunzi wa wimbo huo lakini hilo lilikataliwa.
''Lakini kila nilipousikiza wimbo huu,,nafasi yangu iliniandama ,,wimbo huu ni wangu kwanzia mwanzo hadi mwisho''Alisema Braham.
Hii itakuwa kesi ya pili dhidi ya mwanamuziki huyo juma hili.
Bwana mmoja DJ huko Marekani David Mueller amemshtaki kwa kudai alimsingizia kuwa alimpapasa.
Mueller anataka fidia kwani anasema siye aliyepapasa Swift bali ni bosi wake.
Alikasirika na kwenda mahakamani baada ya kufutwa kazi na kituo cha redio cha KYGO kilichoko Denver.
Comments
Post a Comment