Kijana Lucas alikuwa ni kijana mtanashati na akiwa na umri mdogo kabisa wa miaka 32 alibahatika kuwa na mafanikio makubwa sana, kwani katika umri huo aliokuwa nao tayari alikuwa na biashara zake ambazo zilikuwa zikifanya vizuri sana na alikuwa na kampuni yake ambayo ilikuwa ikisimamia biashara zake hizo. Kampuni yake hiyo ilikuwa kubwa kiasi na pia ilikuwa ikifanya vizuri sana huku yeye mwenyewe Lucas ndio akiwa msimamizi mkuu na mkurugenzi mkuu wa kampuni yake hiyo.
Siku moja Lucas akiwa ofisini kwake akiendelea na shughuli zake za kila siku mara alipokea simu kutoka kwa mke wake aliyekuwa akiitwa Nancy ambaye alimwambia kuwa anaomba sana siku hiyo aende kumchukua kazini kwake kwani gari lake lilikuwa limekorofisha na hivyo alikuwa amemuita fundi aliangalie na baada ya fundi huyo kuja na kuliangalia ameondoka nalo na kwenda nalo gereji kwani fundi huyo amemwambia kuwa ubovu wa hilo gari ni mkubwa kidogo hivyo uwezekano wa gari lake hilo kupona siku hiyo ulikuwa ni mdogo sana. Lucas alimkubalia mke wake na kumwambia kuwa ataenda kumpitia saa kumi na moja jioni hapo ofisini kwake na baada ya kuongea na mke wake huyo, Lucas aliendelea na kazi zake kama kawaida.
Ilivyofika saa kumi kamili Lucas alitoka ofisini kwake na kuanza safari ya kwenda kazini kwa mke wake kumchukua kama walivyokuwa wamekubaliana na pia Lucas alijua kabisa hiyo saa moja ilikuwa ikitosha kabisa kwa yeye kufika kazini kwa mke wake saa kumi na moja kama walivyokuwa wamekubaliana kwenye simu.
Ingawa kulikuwa na foleni kidogo, Lucas hakuwa na wasiwasi kabisa kwani alikuwa ametoka ofisini kwake muda mzuri na alikuwa na saa moja nzima ya kuwa barabarani kwani alikubaliana na mke wake Nancy afike kumchukua kazini kwake saa kumi na moja jioni.
Lucas alifika kazini kwa mke wake Nancy saa kumi na moja na dakika kama kumi hivi ya jioni na alivyofika alimkuta mke wake Nancy akiwa tayari anamsubiri na alikuwa amesimama nje ya ofisi zao. Alivyosimamisha gari karibu na mahali alipokuwa amesimama mke wake Nancy, mke wake huyo alifungua mlango wa gari sehemu ya mbele kwa dereva na kabla hajapanda kwenye gari alimwambia mume wake Lucas kuwa kuna mtu huyo hapo anaomba lifti kwani anasema kuwa eti anakwenda maeneo wanayokwenda wao. Lucas bila hata ya kuuliza zaidi alimwambia mke wake Nancy kuwa sawa hamna shida amwambie tu huyo mtu aingie kwenye gari.
Baada ya Lucas kumjibu hivyo Nancy, Nancy alimwambia huyo mtu kuwa aje tu wampe hiyo lift na baada ya Nancy kumwambia hivyo huyo mtu, huyo mtu alipanda kwenye gari kiti cha nyuma na Lucas aliondoa gari.
Wakiwa wameshakwenda mwendo wa dakika kadhaa Lucas alimuuliza mtu huyo ambaye alikuwa ni mwanaume na mwenye muonekano wa kawaida tu kuwa je yeye anaelekea wapi? Huyo mtu alimjibu Lucas na kumtajia sehemu anayoelekea ambayo ndio ilikuwa njia wanayoipita wao. Lucas alinyamaza na kuendelea kuendesha gari lakini ghafla alishangaa akiona anapigwa loba huku sauti kutoka nyuma ikimwambia kuwa atulie hivyo hivyo na aendelee kuendesha gari kwa utulivu huku akifata maelekezo yake kwani akileta tu ubishi anamuulia mbali hapo hapo.
Nancy ambaye alikuwa amekaa mbele kwenye kiti cha abiria pembeni ya mume wake Lucas ambaye ndio alikuwa akiendesha gari naye alichanganyikiwa kabisa na wala hakujua cha kufanya na hivyo Lucas kwa kujitetea alianza kumwambia huyo mtu kuwa anaomba sana asimdhuru kwani atampa chochote atakachokitaka kutoka kwake. Baada ya Lucas kumwambia hivyo huyo mtu, huyo mtu alimjibu Lucas na kumwambia kuwa yeye hataki chochote kutoka kwake bali anaitaka roho yake tu basi hivyo kwasasa asifanye vurugu yoyote bali asikilize kila anachomwambia na atii kwa utulivu.
Wakati yote hayo yakiendelea huyo mtu alimgeukia Nancy na kumwambia kuwa na yeye anyamaze kimya kwani akipiga kelele yoyote au akifanya vurugu yoyote atamfumua ubongo wake na baada ya kusema hivyo huyo mtu alichomoa bastola na hivyo kufanya Nancy ashindwe cha kufanya na hivyo alibaki tu akitetemeka mpaka karibia mkojo kumtoka. Kibaya zaidi gari la Lucas lilikuwa lina vioo vyeusi hivyo kupelekea watu wa nje kutoweza kuona chochote kilichokuwa kinaendelea humo ndani ya gari.
Baada ya huyo mtu kuchomoa bastola na kumwambia Lucas kuwa atulie na aendeshe gari kwa utulivu huku akisikiliza na kutii maagizo kutoka kwake, huyo mtu alianza kumwambia Lucas kuwa aende njia ambayo alikuwa akimuelekeza yeye. Na wakati hayo yote yakiendelea, Lucas aliwaza kuwa hapo asipotumia akili yake ya kuzaliwa huyo mtu atamuua kweli, hivyo baada ya kuwaza hivyo Lucas akawa anafikiria nini cha kufanya. Huku mke wake Nancy akiwa anatetemeka na hajui cha kufanya, Lucas alijikuta akifungua vioo vya gari hilo kwa haraka sana na huku akiendesha kwa mkono mmoja alipiga kelele kuomba msaada. Watu waliokuwa nje walikuwa wakishangaa kinachoendelea na wala hawakuelewa kabisa hivyo baada ya Lucas kufungua vioo ili kuomba msaada huyo mtu alimpiga Lucas risasi ya kwenye bega la kulia huku akimwambia kuwa si anajifanya mjanja, sasa badala ya kwenda kumuulia huko alikokuwa akimpeleka anamuulia pale pale.-
Baada ya huyo mtu kumpiga risasi Lucas kwenye bega lake la kulia, Lucas alijikuta akishindwa kushikilia mskani wa gari kwa maumivu aliyoyapata na matokeo yake gari lilianza kuyumba yumba, na akiwa bado kwenye siti ya nyuma huyo mtu alijitahidi kushika mskani huo wa gari ili kujaribu kuiendesha yeye mwenyewe lakini gari hilo tayari lilikuwa limeshapoteza uelekeo na hivyo likaacha njia na kupinduka. Huyo mtu alivyoona hilo gari limepinduka, kwa kiwewe alichokipata wala hakufikiria tena kummaliza Lucas hivyo alijitahidi kutoka kwenye gari hilo kwa haraka huku akisaidiwa na watu waliokuwa wamefika kushuhudia ajali hiyo. Watu walianza kukusanyika kuona ajali hiyo na huku watu wakiwa hawaelewi kinachoendelea pikipiki ilikuja kasi na kusimama mahali hapo ambapo gari la kina Lucas lilikuwa limepinduka na huyo mtu ambaye alikuwa amepata michubuko kidogo alipanda kwenye pikipiki hiyo na baada ya mtu huyo kupanda tu kwenye pikipiki hiyo, dereva wa pikipiki hiyo aliiondoa pikipiki hiyo mahali hapo kwa mwendo wa kasi sana, na hivyo aliacha watu wakijiuliza kulikoni? Mbona huyo mtu amewaacha wenzake waliokuwemo wote kwenye gari hiyo iliyopinduka na yeye kupanda pikipiki na mwenye pikipiki kuondoka kwa kasi sana wakati watu wakiendelea kuwaokoa wenzake hao?
Watu wakiwa bado hawaelewi kinachoendelea na bado wakiwa wanashangaa kwanini mmojawapo wa abiria aliyekuwa kwenye gari hilo lililopinduka amepanda kwenye pikipiki na kuondoka mahali hapo, watu hao walianza kuwasaidia Lucas na Nancy kutoka kwenye gari na kwa mshangao wao waliona Lucas akiwa anavuja damu sana kwenye bega lake la kulia na Nancy ambaye alikuwa na michubuko ingawa alikuwa hajaumia sana.
Wakati watu waliofika kuwasaidia kina Lucas wakiendelea kuwasaidia Lucas na Nancy baada ya kuwatoa kutoka kwenye gari lao hilo lililopinduka, Nancy alikuwa akilia huku akisema kuwa amekimbia yule amekimbia. Na watu walivyojitahidi kumuuliza Nancy kuwa kwani yule ni nani kwao? Nancy huku akiendelea kulia alisema kuwa yeye wala hamjui huyo mtu kwani alikuwa tu amewaomba lifti.
Polisi walifika eneo hilo la tukio na walianza kumuuliza Nancy maswali mawili matatu. Nancy aliwaambia mapolisi hao kuwa kwasasa hawezi kusema chochote bali anachoomba tu kwanza mume wake Lucas asaidiwe kupelekwa hospitali kwani alikuwa akivuja damu nyingi sana baada ya kupigwa risasi hiyo ya begani na mtu yule. Hivyo Nancy na Lucas walienda polisi na Nancy aliyekuwa na nguvu kidogo aliandikisha kilichotokea na Lucas ambaye alikuwa amezidiwa alisaidiwa kupelekwa hospitali na alivyofikishwa hospitali madaktari walijitahidi kuiondoa risasi kutoka begani kwa Lucas na walisema kuwa ingawa risasi hiyo ilikuwa imeingia sana lakini wamefanikiwa kuitoa baada ya kumfanyia Lucas upasuaji na hivyo Lucas alilazwa ili kuuguza kidonda chake hospitalini hapo.
Lucas alilazwa, siku ya tano tangu alazwe Lucas alianza kupata nafuu na nguvu kidogo na alianza kuongea pia. Familia ya Lucas ilikuwa bega kwa bega katika kumuuguza Lucas, hivyo hospitalini hapo alikuwepo mke wake Nancy ambaye alikuwa akilala naye na kumuuguza Lucas, pia Nancy alikuwa akisaidiwa na wazazi wake pamoja na wadogo zake wawili waliokuwa wakiitwa Julia na Anthony. Pia kaka yake Lucas aliyekuwa akiitwa Thomas pamoja na mke wake nao walikuwa bega kwa bega kumsaidia Nancy kumuuguza Lucas.
Huko polisi nako, maaskari upelelezi Gabriel na Saidi ambao walikuwa ni maaskari wa upelelezi wa kutumainiwa kabisa waliitwa ofisini kwa bosi wao wa kitengo cha upelelezi askari wa upelelezi Jamal ambaye walivyofika na kuingia ofisini, bosi wao huyo aliwaambia kuwa amewaita kwani kuna kesi hapo anataka waishughulikie.
Askari upelelezi Jamal aliwaambia maaskari wa upelelezi Saidi na Gabriel kuwa kuna mfanyabiashara mmoja ambaye ameanza kuwa maarufu sana siku za hivi karibuni sasa siku kadhaa zilizopita alivamiwa na jambazi lakini cha ajabu huyo jambazi hakuonyesha nia yoyote ya kutaka kumpora gari au kuchukua kitu chochote kutoka kwake bali inaonyesha alitaka roho yake na alimwambia hivyo kuwa anaitaka roho yake na hiyo ni kwa mujibu wa mke wa mfanyabiashara huyo ambaye alihojiwa kwa haraka haraka anachokumbuka kilichowapata yeye na mume wake siku hiyo na ndio akawaeleza hivyo, tena cha kushangaza ndani humo kwenye gari mfanyabiashara huyo alikuwa na shilingi milioni moja na simu za gharama lakini huyo mtu wala hakutaka kabisa kuchukua kitu chochote kati ya hivyo na aliendelea kusisitiza kuwa anaitaka roho ya huyo mfanyabiashara huyo mpaka pale walivyopata ajali na anaona walipata ajali hiyo kwasababu ya purukushani kati ya huyo mfanyabiashara na huyo jambazi sasa baada ya kupata maelezo ya juu juu kidogo kutoka kwa mke wa mfanyabiashara huyo ameona angalau kuna mwanga wa pa kuanzia kesi hiyo na hivyo ameona awakabidhi wao faili la kesi hiyo na anataka majibu ya haraka sana na pia atapenda sana kama watakuwa wakimpa maelezo ya kesi hiyo angalau mara moja au mbili kwa wiki na baada ya bosi wao Jamal kuwaambia hivyo maaskari upelelezi Saidi na Gabriel aliwakabidhi faili la kesi hiyo na kuwaambia kuwa anawatakia kazi njema na anasubiri majibu ya haraka na ya kuridhisha kuhusu kesi hiyo.
Maaskari upelelezi Saidi na Gabriel baada ya kupokea faili hilo walianza kuliangalia faili hilo kwa zamu na kwa haraka haraka, na askari upelelezi Saidi alimwambia bosi wake huyo kuwa hiyo kesi kwao ni rahisi sana na wanachohitaji ni vitendea kazi tu, pia wafanyabiashara wengi mara nyingi huwa hawapendani wenyewe kwa wenyewe na pia mara nyingi huwa wanadhulumiana sana hivyo inawezekana huyo mtu aliyetaka kumuua Lucas labda itakuwa ametumwa na mahasimu wake wa kibiashara hivyo ukweli utajulikana tu.
SEHEMU YA PILI

Comments
Post a Comment