Hadithi Lucas 10

Sehem ya - 10

Muda wa kuangalia mahabusu ulivyokwisha mama yake Nancy aliondoka kurudi nyumbani kwake. Alivyofika tu nyumbani kwake alimkuta mwanae Julia akiwa sebuleni akiangalia TV, na alivyomuona tu mama yake, Julia alianza kutabasamu na alimwambia mama yake kuwa Rehema amempigia simu tena na amemwambia kuwa Fatuma ameachiwa huru na mapolisi na kwasasa yule mwanamke anayeishi na Lucas ndio amekamatwa na polisi na mpaka sasa bado anashikiliwa huko kituoni.

Baada ya Julia kumwambia hivyo mama yake, mama yake Nancy alimwambia mwanae huyo kuwa hebu ngoja kwanza mbona anamchanganya lakini! Hebu ngoja kwanza akae chini kwenye kochi ndio amuelezee vizuri.

Baada ya-mama yake Nancy kusema hivyo alikaa kwenye kochi na kujifuta jasho kwa kitambaa chake cha mkononi alichokuwa nacho halafu akamwambia mwanae Julia kuwa hebu aendelee sasa kumuelezea kwa utaratibu alivyoambiwa na Rehema kwenye simu.

Julia alianza kumwambia tena mama yake kama alivyokuwa amemwambia mwanzo na alivyomaliza alisema kuwa yani yeye amefurahi sana kupita maelezo huyo mwanamke kukamatwa maana alivyoingilia ndoa ya dada yake alifikiri nini na tena hata kama itagundulika yeye hana makosa lakini cha moto atakuwa amekiona hivyo hata hiyo nyumba ataiona chungu.

Baada ya Julia kusema hivyo, mama yake Nancy alimuuliza Julia kuwa je Rehema kamwambia kuwa kwanini wameamua kumuachia Fatuma na wameamua kumkamata huyo mwanamke? Julia huku akiendelea kutabasamu alisema kuwa Rehema hajamwambia sababu iliyopelekea Fatuma kuachiwa na huyo mwanamke kukamatwa kwani alivyomuuliza alisema hata yeye hajui ila akipata habari nzuri zaidi atampigia na kumwambia.

Baada ya Julia kusema hivyo, mama yake Nancy aliguna na alianza kusema kuwa inawezekana hapa katikati kuna kitu na kuna mchezo unaochezeka ambao aidha Lucas yeye mwenyewe anaujua au haujui, hivi inakuaje kweli kila mwanamke anayeishi naye anakamatwa kwa kuhusishwa kutaka kumuua Lucas!? Ni kweli hawa wake zake wanataka kumuua!? Ni kweli na mwanae Nancy naye alitaka kumuua!? Na hata kama ni kweli wanataka kumuua, je ni kwasababu gani hasa!? Mbona kama mali na utajiri kuna watu wenye mali nyingi sana na utajiri wa kutupa ambao hata yeye Lucas wala hawafikii hata kidogo lakini hawajawahi kutaka kuuliwa na wake zao!?

Baada ya mama yake Nancy kusema hivyo, Julia mdogo wake Nancy alibaki kumtazama mama yake na kumshangaa huku akimwambia kuwa yani anashangaa nini sasa huyo mwanamke kukamtwa au!? Yani anamuonea huruma mtu ambaye alitaka kuivunja ndoa ya mwanae Nancy!? Kweli anashangaza! Yani yeye alifikiri atazifurahia hizi habari lakini matokeo yake eti anamsikitikia mbaya aliyetaka kumvunjia mwanae ndoa yake!
Mama yake Nancy alimuangalia Julia halafu akasema kuwa hata kama huyo mwanamke sijui ameingilia ndoa ya mtoto wake Nancy lakini mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni, kwani kinachomtatiza hapo yeye ni kuwa hivi kwa mali gani hasa alizokuwa nazo huyo Lucas mpaka kila mwanamke atake kumuua yeye!?

Baada ya mama yake Nancy kusema hivyo, Julia alianza kumwambia mama yake huyo kuwa hee kwahiyo utajiri na umaarufu wa Lucas yeye haujui!? Kama anajifanya yeye amesahau utajiri wa Lucas basi ngoja yeye Julia amkumbushe ni kuwa Lucas anayesema ana utajiri gani basi mwenzie ana kampuni na ameajiri watu kibao mpaka wasomi wenye elimu zao ambao wengine wamemzidi hata yeye mwenyewe Lucas kwa elimu, pia Lucas ana nyumba hiyo anayoishi, ana magari ya kutembelea ya kifahari, na sasa anajenga bonge la ghorofa la maana, pia ana viwanja na mashamba karibia kila sehemu na bado utajiri wake mwingine wao hawaufahamu na mambo yake yanazidi kumnyookea siku hadi siku halafu yeye anasema ana utajiri gani!? Yani wanamdharau tu Lucas sasa kwasababu ya hayo matatizo yaliyotokea kati yake na dada yake Nancy lakini kwasasa shemeji yake huyo ni maarufu na kila mtu anajua kuwa Lucas ana pesa ingawa hawezi kuwafikia hao matajiri wakubwa kwenye nchi hii hivyo lazima huyo mwanamke atakuwa ameingia tu tamaa ili apate hizo mali baada ya kuona hizo hila zake za kutaka kumzalia Lucas mtoto zimeshindikana baada ya mimba zake kuwa zinatoka mara kwa mara.

Baada ya Julia kusema hivyo, mama yake alimwangalia na kusema kuwa haya anakubaliana naye kuwa huyo mwanamke alitaka kumuua Lucas sababu ya mali je na dada yake Nancy naye je!?-Kwahiyo naye ni kweli ndio alimkodia yule mtu aliyewavamia ili amuue huyo Lucas ili naye apate hizo mali kama watu wengi wanavyodhani si ndio!?-
Baada ya Julia kumwambia mama yake kuwa huyo mwanamke-aliyekuwa anaishi na Lucas atakuwa ameingia tu tamaa ya kupata mali za Lucas ndio maana akataka kumuua Lucas ili apate hizo mali baada ya kuona hizo hila zake za kutaka kumzalia Lucas mtoto zimeshindikana baada ya mimba zake kuwa zinatoka mara kwa mara, mama yake alimwangalia na kusema kuwa haya anakubaliana naye kuwa huyo mwanamke alitaka kumuua Lucas sababu ya mali je na dada yake Nancy naye je!? Kwahiyo naye ni kweli ndio alimkodia yule mtu aliyewavamia ili amuue huyo Lucas ili naye apate hizo mali kama watu wengi wanavyodhani si ndio!?

Baada ya mama yake Nancy kumuuliza mwanae Julia kuwa kwahiyo hata dada yake Nancy naye ndio aliyemkodia mume wake Lucas watu ili wamuue sababu ya mali kama watu wengi wanavyodhani na kama anavyoambiwa sasa Stella huyo mwanamke mwingine wa Lucas, Julia alimwambia mama yake kuwa ana uhakika asilimia mia moja kuwa dada yake Nancy hakupanga kumuua huyo Lucas ila kosa alilolifanya dada yake huyo ni kumuombea lifti huyo mtu aliyetaka kumuua Lucas wakati hamjui mtu huyo, lakini ana uhakika kabisa kuwa huyo mwanamke yeye hajasingiziwa bali ni kweli ndio alitaka kumuua Lucas.

Baada ya Julia kumwambia hivyo mama yake, mama yake Nancy alimuuliza mwanae huyo kuwa hebu ampe sababu zinazomfanya aamini kuwa huyo mwanamke aliyekuwa anaishi na Lucas baada ya Nancy kukamatwa na polisi ndiye aliyetaka kumuua Lucas kwa kumuwekea sumu kwenye chakula lakini dada yake Nancy ingawa naye anashtakiwa kwa kosa kama hilo hilo yaani la kutaka kumuua Lucas yeye ndio amesingiziwa na siyo yeye aliyemtuma yule mtu ili amuue Lucas.

Baada ya mama yake Nancy kumuuliza hivyo mwanae Julia, Julia alimwambia mama yake kuwa sababu kubwa hasa inayomfanya yeye aamini dada yake Nancy hakutaka kumuua mume wake Lucas bali amebambikiziwa tu hiyo kesi ni kuwa sababu ya kwanza yeye ni mke wa ndoa wa Lucas sasa amuue huyo Lucas kwa lipi wakati anajua kabisa hizo mali za mume wake ni za kwao wote na isitoshe yeye pia amechangia kwa kiasi fulani kwenye hizo biashara za mumewe!? na pia sababu ya pili ni kuwa dada yake Nancy amezaa mtoto na mume wake huyo sasa hata ingetokea wameachana na mume wake huyo tayari kulikuwa na muunganiko wa yeye na Lucas kupitia mtoto wao huyo yaani Henry hivyo kwa vyovyote mali za mwanae Henry ni za kwake pia sasa kwa kweli inakuwa ngumu sana kwake kumfanyia hivyo baba wa mtoto wake na hilo mtu yeyote anaweza kulithibitisha, kwani hata wakienda mahabusu kumuangalia mara nyingi sana yeye akianza kumueleza mambo ya Lucas na kama kuna mabaya yamemfikia Lucas dada yake huyo huwa hapendi kabisa akimueleza kuhusu Lucas kupatwa na mabaya na huwa anasema wasifurahie kama Lucas amepatwa na mabaya kwani huyo ni mume wake wa ndoa na pia ni baba wa mtoto wake Henry hata kama kwasasa amemgeuka kiasi hicho na kumuona yeye ndio aliyetaka kumuua lakini wasifurahie anapopatwa na mabaya. Julia aliendelea kumwambia mama yake kuwa na sababu kubwa hasa inayomfanya aamini kuwa huyo mwanamke aliyekuwa anaishi na Lucas yeye alitaka kumuua Lucas na hasingiziwi ni kuwa kwanza huyo mwanamke anajua kabisa yeye sio mke wa ndoa wa Lucas na ni mpita njia tu sasa dada yake Nancy akionekana hana hatia na akiachiwa huru yeye itakuaje!? Je atakwenda wapi!? Kibaya zaidi huyo mwanamke amejaribu sana kushika mimba lakini mimba zote zinatoka sasa bora hata angekuwa amezaa mtoto na Lucas labda naye angekuwa na mgao wa hizo mali hivyo labda kwa kuliona hilo akaona bora amuulie tu mbali huyo Lucas ili yeye achukue chake mapema halafu asepe zake.

Baada ya Julia kumwambia hivyo mama yake, walibaki tu kubishana mpaka baba yake Nancy na Anthony nao wakaja na wakawauliza wanabishana nini? Mama yake Nancy na Julia wakawaambia kuwa Rehema amempigia tena simu Julia na amemwambia kuwa Fatuma ameachiliwa huru na sasa yule mwanamke aliyekuwa anaishi na Lucas ndio amekamatwa na polisi hivyo na wao ndio wanabishana hapo kwani Julia anasema kuwa itakuwa kweli huyo mwanamke anahusika kutaka kumuua Lucas labda ili achukue yeye hizo mali zake na mama yake anamkatalia kwani anasema kama huyo mwanamke alitaka kumuua Lucas -ili achukue hizo mali zake na Nancy je itakuwa ni kweli naye alitaka kumuua Lucas ili naye achukue mali zake kama watu wengi wanavyodhania na hivyo Nancy hajasingiziwa? Hivyo ndio wanachobishania hicho.

Baada ya baba yake Nancy na Anthony kuelezwa wanachobishania mama yao na Julia nao walibaki kusema kuwa kweli hapo ni pagumu kusema kuhusu huyo mwanamke kama anahusika au hausiki hivyo inabidi tu wawaachie polisi wenyewe ndio watajua ukweli uko wapi na pia labda waendelee kusikilizia sababu hasa iliyofanya polisi kumuona huyo mwanamke labda naye atakuwa anahusika mpaka kuamua kumuachia Fatuma na kumshikilia yeye.

Pia baba yake Nancy aliendelea kusema kuwa ila hivi huyo mwanamke naye atakuwa ni mjinga kiasi gani mpaka akaamua kufanya hilo kosa la kutaka kumuua Lucas wakati akijua kabisa mke wa Lucas yupo polisi kwa kosa kama hilo, kweli haya mambo ya Lucas kutaka kuuliwa na wanawake anaoishi nao ni utata mtupu!

Baada ya baba yake Nancy kusema hivyo, mama yake Nancy alidakia na alianza kumwambia mume wake huyo kuwa bora hata yeye ameliona hilo kwani hata yeye ndio alikuwa akisema hivyo hivyo halafu Julia akawa anambishia na kusema kuwa eti mbona anamtetea huyo mwanamke wakati ameingilia ndoa ya mwanae. Kwani hata yeye mama yake Nancy amejiuliza sana tena sana swali kama hilo la kwake ya kuwa hivi huyo mwanamke atakuwa ni mjinga na mpumbavu kiasi gani kurudia kosa hilo hilo ambalo mwenzake anashtakiwa nalo tena hata kabla muda mrefu haujapita kwani ni miaka mitatu tu na miezi kadhaa tangu tukio la mwanzo litokee na hata watu na huyo Lucas mwenyewe bado hawajasahau kwani hata hiyo hukumu ya Nancy mwanae bado haijatoka.

Baada ya mama yake Nancy kusema hivyo, baba yake Nancy alibaki kuguna tu na akasema kuwa kwa kweli haya mambo ni magumu sana na ni polisi wenyewe ndio watakaotatua kitendawili hicho ingawa yeye kama mzazi anaona uwezekano wa aidha mtoto wake Nancy kuachiwa huru kama hana hatia au kufungwa kabisa.

Wazazi wake Nancy na wadogo zake waliendelea kuongea huku mama yake Nancy akisema kuwa anatamani sana kesho ifike ili aende mahabusu akamueleze Nancy kuhusu hayo yanayotokea huko kwa Lucas ya kuwa sasa Fatuma ameachiwa huru na badala yake yule mwanamke aliyekuwa anaishi na Lucas yeye ndio amekamatwa.

Kesho yake ilifika na mama yake Nancy akiongozana na Julia walikwenda kumuona Nancy. Walivyofika walianza kumueleza Nancy mambo yote yanayoendelea huko kwa Lucas na Nancy aliwaambia kuwa amefurahi sana kusikia kuwa Fatuma ameachiwa huru kwani alitaka kushangaa kimempata nini Fatuma mpaka kuamua kufanya hivyo kwani kwa muda wote aliokaa na Fatuma pamoja na Rehema anawafahamu vizuri sana wasichana hao ndio maana mwanzo mama yake alivyomwambia kuwa Fatuma amekamatwa kwa kosa la kumwekea sumu Lucas kwenye chakula yeye alishangaa sana.

Pia Nancy aliendelea kusema kuwa kuhusu huyo mwanamke aliyekuwa akiishi na Lucas naye kukamatwa kwa kosa hilo la kutaka kumuwekea sumu Lucas hana la kusema kwani hajui kama ni kweli huyo mwanamke atakuwa amefanya hivyo au naye amesingiziwa kama alivyosingiziwa yeye.

Baada ya Nancy kusema hivyo alimuuliza mdogo wake Julia kuwa sasa Rehema alivyompigia simu hajamwambia sababu yoyote iliyopelekea polisi kumuhisi huyo mwanamke kuwa ndio atakuwa amefanya kitendo hicho? Julia alimwambia dada yake Nancy kuwa Rehema hajamwambia sababu iliyopelekea huyo mwanamke kukamatwa kwani alivyomuuliza alisema hata yeye hajui ila akipata habari nzuri zaidi atampigia na kumwambia.

Baada ya Julia kumjibu hivyo Nancy, Nancy aliguna tu na kusema haya watasikia tu kinachoendelea.

Siku hiyo mama yake Nancy, Julia na Nancy mwenyewe waliongea sana mpaka muda wa kuangalia mahabusu ulivyokwisha ndio mama yake Nancy pamoja na Julia wakaondoka zao.

Wakati familia ya Nancy wakisubiria kujua kinachoendelea huko kwa Lucas, huko polisi nako walianza kumuhoji Stella mwanamke aliyekuwa anaishi na Lucas kuhusu sababu za kutaka kumuua Lucas kwa kumuwekea sumu kwenye chakula.

Sababu kubwa iliyopelekea polisi kumkamata Stella na kuanza kumuhoji ni kuwa...
Wakati familia ya Nancy wakisubiria kujua kinachoendelea huko kwa Lucas, huko polisi nako walianza kumuhoji Stella mwanamke aliyekuwa anaishi na Lucas kuhusu sababu za kutaka kumuua Lucas kwa kumuwekea sumu kwenye chakula.

Sababu kubwa iliyopelekea polisi kumkamata Stella na kuanza kumuhoji ni kuwa siku hiyo Lucas aliyowekewa sumu kwenye chakula Rehema mmojawapo wa wasichana wa kazi wa Lucas aliomba ruhusa kwa mabosi wake hao kuwa anakwenda mjini kuwatumia wazazi wake pesa za matumizi na pia alivyotoka huko alikwenda kujinunulia mahitaji yake yeye mwenyewe kama nguo na vitu vingine na alirudi jioni na Lucas naye alikuwa amekwenda kazini kwake. Kwahiyo siku hiyo alibaki Fatuma na Stella mwanamke aliyekuwa anaishi na Lucas peke yao, na Fatuma siku hiyo ndio alipika chakula na aliandaa chakula mezani kwa ajili ya Stella na pia alijipakulia chakula chake na kula. Walivyomaliza kula Fatuma aliosha vyombo walivyolia na kwenda kupumzika chumbani kwake na Stella naye alikwenda kupumzika chumbani kwao. Ilivyofika mida ya saa tisa jioni Lucas alirudi na Stella alimuita Fatuma ili akamuwekee chakula Lucas, hivyo Fatuma alitoka chumbani alipokuwa amejipumzisha na kwenda kuandaa chakula mezani kwa ajili ya Lucas.

Wakati Fatuma akiwa anamuandalia Lucas chakula, Lucas na Stella wao walikuwa wapo sebuleni wanaangalia TV, na baada ya dakika kadhaa kupita Lucas alibadilisha channel na kuweka kituo cha TV ambacho kilikuwa kinaonyesha mpira huku akimwambia Stella kuwa siku hiyo timu yake ilikuwa ikicheza na timu pinzani. Baada ya Lucas kubadilisha channel na kuanza kuangalia mpira Stella ambaye alikuwa naye hapo sebuleni huku akinywa kinywaji chake taratibu alimwambia Lucas kuwa aende akale kwanza kabla chakula hakijapoa kuliko kupoteza muda kwa kuangalia mpira kwani anamfahamu yeye alivyo kwa jinsi anavyopenda mpira hata kula atasahau kabisa. Baada ya Stella kumwambia hivyo Lucas, Lucas alimwambia Stella kuwa kwa jinsi mpira ulivyo mtamu ngoja kwanza aendelee kuangalia mpaka kieleweke na ajue hatma ya timu yake aliyokuwa akiishabikia ndio atakwenda kula hivyo asiwe na wasiwasi kwani atakula tu.

Lucas aliendelea kuangalia mpira huku Stella akimkumbushia mara kwa mara kuwa aende akale kwani chakula kitapoa na Lucas naye alikuwa akimjibu Stella kuwa ngoja kwanza asubiri mpaka timu yake itakapokuwa na matokeo mazuri ndio ataenda kula hivyo Lucas aliendelea kuangalia mpira na hakwenda mezani kula mpaka mpira ulivyoisha ndio alinyanyuka kwenda kula.

Lucas alivyofika mezani alikuta ma hotpot manne ambapo kulikuwa na wali, nyama ya mchuzi, mboga ya majani na kuku wa kukaanga. Na alivyofungua tu hotpot ya wali alikuta wali umebadilika rangi kwani ulikuwa na rangi ya njano na kijani hivyo akashtuka kidogo na akamuuliza Stella kuwa mbona wali una rangi ya njano na kijani kwani wameweka zile rangi za chakula zinazowekwa kwenye wali ili kuubadilisha rangi!? Stella alipatwa na kigugumizi kidogo na alishindwa hata kujibu hivyo alimwambia Lucas kuwa yeye hajui kwani yeye hajapika hicho chakula hivyo aulizwe Fatuma ambaye ndio amepika hicho chakula. Baada ya majibu hayo ya Stella, Lucas alimuita Fatuma na kumuuliza kuwa leo ameamua kuwapikia chakula chenye rangi? Fatuma akamjibu na kusema hapana mbona amepika tu wali wa kawaida. Majibu hayo ya Fatuma yalimshtua kidogo Lucas na kumfanya awe na mashaka hivyo akamuita na Stella ambaye muda wote huo ambao Lucas alikuwa akishangaa kuhusu hicho chakula yeye alikuwa amekaa sebuleni kwenye kochi akinywa kinywaji chake alichokuwa akinywa muda wote. Stella alivyofika hapo alivyokiona hicho chakula naye alishangaa sana na hivyo wote kwa pamoja walianza kuulizana itakuwa ni nini hicho? Wakati wote wakiendelea kushangaa, Lucas alifungua hotpot lililokuwa na nyama ya mchuzi na mchuzi nao ulikuwa wala haueleweki rangi yake kwani ulikuwa kama wa bluu na pia kama wa kijani ndio hapo Lucas akamuweka kitimoto Fatuma na kumuuliza kulikoni hivyo vyakula vina rangi ya ajabu wakati anasema hajaweka rangi yoyote!?

Baada ya Lucas kumuuliza hivyo Fatuma, Fatuma aliendelea kusisitiza kuwa hicho chakula amepika yeye lakini hajaweka kitu chochote cha kubadilisha rangi -kwenye chakula.

Baada ya Fatuma kumjibu hivyo Lucas, Lucas alifungua hotpot iliyokuwa na mboga za majani na kuku wa kukaanga lakini humo hakuona chochote na wala hazikuwa na rangi yoyote bali zilikuwa ni mboga tu za kawaida kama siku zote. Hivyo Lucas aliamua kunusa huo wali na mchuzi na aligundua kuna harufu isiyo ya kawaida ingawa ilikuwa ni kwa mbali sana na sio rahisi kuigundua kama mtu pua zake haziko vizuri sana hivyo pale pale baada tu ya kunusa vyakula hivyo Lucas akaanza kumkazania Fatuma kuwa lazima atakuwa ameweka kitu humo kwenye wali na nyama ya mchuzi kwani hizo rangi sio za kawaida kabisa. Fatuma alivyoona Lucas anamkazania kuwa lazima atakuwa ameweka kitu humo kwenye hicho chakula chake, Fatuma alianza kulia na kumwambia Lucas kuwa hapana yeye hajui chochote kuhusu hizo rangi za kwenye hicho chakula kwani wakati anakipakua jikoni na kukiweka mezani kilikuwa cha kawaida kabisa na pia isitoshe yeye na Stella nao wamekula chakula hicho hicho.
SEHEMU YA KUMI NA MOJA 11

Comments