Hadithi Lucas 13

Sehemu ya - 13

Baada ya maaskari wale kumuonyesha Stella kipande cha video kilichokuwa kinamuonyesha akiingia jikoni huku akiwa ananyata na alivyofika huko jikoni alifunua masufuria mawili kwa haraka na kuweka kitu halafu akaondoka tena kwa kunyata na kuelekea sebuleni, na walivyomaliza kumuonyesha Stella hicho kipande cha video na wao kumuuliza kuwa alikuwa anaweka nini humo kwenye hayo masufuria mawili kama alivyoonekana kwenye kipande hicho cha video hiyo na Stella naye kuwajibu kuwa- alikuwa anaweka chumvi, maaskari wale walitabasamu halafu walimwambia Stella kuwa mwanzo aliwaambia kuwa ana uhakika asilimia mia moja kuwa hakuingia kabisa huko jikoni siku hiyo Lucas aliyowekewa sumu kwenye chakula na pia alidiriki mpaka kuapa huku akiwa ameshika Biblia kitabu kitakatifu kwa wakristo ili kuwahakikishia kuwa siku hiyo hakuingia huko jikoni, halafu baada ya kuonyeshwa kipande hicho cha video anaanza kujichanganya kwa kusema kuwa eti mara sio siku hiyo bali ilikuwa ni siku nyingine ingawa alikuwa amevaa nguo hizo hizo, na mara anasema kuwa alikuwa akiweka chumvi sasa kwa taarifa yake hicho kipande cha video kinachomuonyesha akiwa jikoni akiweka vitu kwenye masufuria ilikuwa ni siku ile ile ambayo Lucas aliwekewa sumu kwenye chakula na pia hata hiyo video nayo inaonyesha siku ile aliyowekewa Lucas sumu na tarehe hiyo hapo inaonyesha kuwa ni siku hiyo na baada ya kusema hivyo maaskari wale walimuwekea tena Stella vipande vya video kuonyesha matukio yote yaliyotokea siku ile mpaka yeye Stella alivyotoka jikoni, alivyoelekea maeneo ya bafuni na alivyorudi na kuanza kumuita Fatuma ili aje kumuandalia Lucas chakula na yeye kuchukua kinywaji na kukaa sebuleni, na Stella alivyoona vipande hivyo vya video alibaki kujisemea moyoni kuwa yani kumbe huyo mpumbavu Lucas alikuwa ameweka ma camera kwenye nyumba yake na yeye wala hakulifahamu hilo kweli amepatikana!

Stella aliendelea kusisitiza kuwa alikuwa akiweka chumvi kwenye chakula kile ili angalau labda maaskari wale waweze kumuelewa na asihukumiwe kwani alikuwa ameshachanganyikiwa na wala hakujua tena jinsi ya kujitetea, na wakati akiendelea kusisitiza kuwa alikuwa akiweka chumvi kwenye chakula kile, maaskari wale walimuuliza Stella kuwa kwani yeye alikuwa amekatazwa kuingia huko jikoni mpaka aingie kwa kunyata vile!? Hivyo awaeleze kwanini aliingia huko jikoni kwa kunyata vile na pia hiyo chumvi alitoka nayo wapi!? Maana hakuonekana akichukua chumvi iliyokuwepo pale jikoni na pia hakuonekana kabisa kuonja chakula hicho baada ya kuweka hiyo chumvi anayodai kama wafanyavyo watu wengi wakiwa wanapika na badala yake alionekana akiweka hiyo chumvi anayodai moja kwa moja tena kwa haraka mara tu baada ya kuingia jikoni kuonyesha kabisa kuwa hiyo chumvi anayodai ni chumvi alitoka nayo huko huko alikokuwa ametoka na wala hakutumia chumvi iliyokuwepo pale jikoni, na pia hata kama alikuwa anaweka chumvi kwenye hicho chakula kwanini aongeze chumvi kwenye chakula ambacho hakupika yeye!? na pia kwanini hakuonja baada ya kuongeza hiyo chumvi!? Na pia kwanini akatae kabisa kuwa siku hiyo hakuingia jikoni kabisa wakati aliingia na masufuria alifunua na kuweka hiyo chumvi!? Halafu pia kwenye hizo video ameonekana akifunua masufuria mawili na kuweka hiyo chumvi anayodai wakati ndio hayo hayo masufuria yaliyokutwa yakiwa na hiyo sumu yaani sufuria la wali na sufuria la mboga ya nyama ya mchuzi.

Maaskari wale waliendelea kumuuliza Stella maswali mfululizo kuwa halafu pia hicho chakula si alikula yeye na Fatuma mchana kabla Lucas hajarudi sasa kwanini aje kuongeza hiyo chumvi baadaye? Hivyo hebu awajibu hayo maswali yao yote ambayo wamemuuliza.

Baada ya kuulizwa hivyo Stella alikosa kabisa jibu la kujibu hivyo alibaki akiwa ameinamisha tu kichwa chini.

Maaskari wale pia walimwambia Stella kuwa asiwapotezee muda kwani ushahidi wote wanao na unaonyesha kuwa yeye ndio aliyefanya vile sema walitaka tu kupima kiwango chake cha imani lakini wamegundua kuwa yeye ni mtu hatari sana kwani hata Mungu wake anayemuabudu hamuogopi kabisa, hivyo sasa muda wa kubembelezana na kudanganyana umeshakwisha ila wanachotaka kusikia kutoka kwake ni ukweli mtupu kwa maswali watakayokwenda kumuuliza.

Baada ya maaskari wale kumwambia hivyo Stella, walimuuliza Stella kuwa kwenye kipande kimoja cha video, huku wakimuonyesha kipande hicho, kuwa anaonekana akitoka jikoni halafu kwenye kipande kingine tena cha video huku nacho wakimuonyesha pia anaonekana akirudi sebuleni kutoka jikoni halafu akaelekea maeneo kama ya bafuni au chooni halafu akarudi na kumuita Fatuma ili amuandalie Lucas chakula mezani na yeye akachukua kinywaji na kukaa sebuleni, sasa awaeleze huko bafuni/chooni alikwenda kufanya nini mara tu alivyotoka jikoni? Baada ya kuulizwa swali hilo na maaskari hao Stella alinyamaza kimya na alikataa kata kata kujibu swali hilo.

Baada ya Stella kunyamaza na kukataa kata kata kujibu swali hilo, maaskari hao walimwambia Stella kuwa wao wanajua kabisa kuwa alikwenda huko bafuni/chooni ili kunawa ile sumu aliyokuwa ameishika ili asijisahau akailamba kwenye vidole vyake au akashika chakula akala au pia aliogopa maaskari wangekuja labda angegunduliwa hivyo awaeleze ukweli kule bafuni/chooni alikwenda kufanya nini?

Baada ya kuelezwa vile na maaskari wale, Stella bado aliendelea kunyamaza kimya na hapo ndipo maaskari wale walivyoanza kumtesa Stella mpaka Stella akaanza kupiga kelele kwa maumivu na kuwaambia maaskari wale kuwa wamuache kwani atasema ukweli.

Maaskari wale walimuacha Stella, na Stella naye aliwajibu maswali yao na kusema kuwa ndio ile ni sumu na alivyoenda bafuni alikwenda kuinawa ili isibaki kwenye mikono yake na kugundulika au yeye kushika chakula au kuilamba kwa bahati mbaya.
Wakati maaskari wakiendelea kumuhoji Stella, ofisi ya mkemia mkuu walikokuwa wamepewa jukumu la kuchunguza kile chakula walichohisi kimewekwa sumu walileta ripoti ya majibu yaliyopatikana baada ya kukichunguza chakula hicho na ripoti hiyo ilisomeka kuwa chakula hicho kilikuwa na sumu, na sumu hiyo iliyowekwa kwenye chakula hicho ilikuwa ni sumu kali sana ambayo ina uwezo wa kumuua mwanadamu ndani ya dakika kadhaa yani hata dakika ishirini hazifiki hivyo kama Lucas angekula chakula hicho hata kijiko kimoja tu sasa hivi wasingekuwa naye tena. Na ndio maana chakula hicho kilibadilika rangi muda mfupi baada ya kuwekwa sumu hiyo kuonyesha kuwa sumu hiyo tayari ilikuwa imeshaanza kufanya kazi, na kwasababu Lucas hakula chakula hicho ndani ya muda huo mfupi tangia sumu hiyo iwekwe ndio maana alikuta tayari chakula kimeshabadilika rangi kuonyesha kuwa sumu hiyo tayari ilikuwa imeshaanza kufanya kazi na ilikuwa ikiendelea kufanya kazi tangu ilivyowekwa.

Na pia mtu angekula chakula hicho chenye sumu hiyo hata angepewa tiba gani uwezekano wa kupona ulikuwa haupo kabisa labda kama angekuwa ni malaika aliyeshushwa kutoka mbinguni.

Baada ya ripoti hiyo kutoka ofisi ya mkemia mkuu, maaskari hao walizidi kuwa na shauku ya kutaka kufahamu sababu hasa zilizopelekea Stella kutaka kumuua Lucas hivyo maaskari wale waliendelea kumuhoji Stella na walianza kumuuliza Stella kuwa je kwanini ameamua kufanya hivyo? Baada ya Stella kuulizwa swali hilo alinyamaza kimya na alikataa kata kata kusema chochote na maaskari wale walivyoona Stela amegoma kabisa kusema waliamuru apelekwe kwenye chumba cha mateso kama masaa matatu hivi na akitoka huko ndio waje wamuhoji tena. Hivyo Stella alipelekwa kwenye chumba hicho cha mateso kwa muda huo wa masaa matatu na alivyotoka huko alikuwa nyaka nyaka kwa mateso na maaskari wale walianza kumuhoji tena.

Maaskari wale walimuuliza tena Stella kuwa kwanini alitaka kumuua Lucas kwa kumuwekea sumu kwenye chakula? Stella uzalendo ulikuwa umeshamshinda kwa yale mateso aliyoyapata hivyo huku akiendelea kuugulia maumivu aliwajibu maaskari wale na kuwaambia kuwa alifanya vile kwasababu alikuwa ametumwa kufanya vile na haukuwa uamuzi wake kufanya vile.

Maaskari wale walimwambia Stela kuwa ni bora aendelee kuonyesha ushirikiano kwani asipowapa ushirikiano atapelekwa tena kwenye kile chumba cha mateso na safari hii akienda tena watahakikisha anakaa masaa 6, hivyo awe mtiifu na ajibu maswali yao kwa ufasaha kabisa.

Baada ya maaskari hao kumwambia hivyo Stella, walimuuliza je ni nani huyo aliyemtuma kufanya hivyo?

Stella bila kuficha alimtaja huyo mtu na alisema kuwa ni Thomas ndio aliyemtuma kufanya hivyo.

Stella alivyojibu hivyo, maaskari wale walimuuliza je huyo Thomas ni nani? Ni mfanyabiashara mwenzake na Lucas au? Stella alijibu na kuwaambia maaskari hao kuwa Thomas ni kaka yake na Lucas.

Baada ya Stella kujibu hivyo, maaskari wale walimuuliza Stella na kumwambia kuwa kwahiyo huyo Thomas ni kaka yake Lucas kivipi? Ni binamu yake? au ni mtoto wa shangazi yake au mjomba wake? au ni mtoto wa mama yake mkubwa au mama yake mdogo? Stella naye bila hata ya kupepesa macho aliwajibu maaskari hao na kuwaambia kuwa Thomas ni kaka yake wa damu na Lucas yaani ni baba mmoja mama mmoja na wamezaliwa wawili tu wa kwanza ni Thomas kwa kuzaliwa -na wa pili ambaye pia ni wa mwisho ni Lucas.

Baada ya jibu hilo la Stella maaskari hao wote walibaki wakitazamana kwa mshangao!

Baada ya Stella kuwaambia maaskari wale kuwa aliyemtuma kuweka sumu kwenye chakula cha Lucas ni Thomas ambaye ni kaka wa damu wa Lucas na maaskari hao wote kubaki wakitazamana kwa mshangao, kilipita kimya kwa muda bila ya mtu yeyote kusema kitu chochote kuonyesha kila mtu alikuwa akitafakari lile jibu la Stella.

Baada ya dakika kadhaa kupita, mmoja wa maaskari wale alimwambia Stella kuwa ana uhakika na anachokisema au anataka tu kuwagombanisha ndugu tena wa damu? Stella alisisitiza kuwa anachosema ni ukweli mtupu kabisa na wala hadanganyi au kumsingizia mtu yeyote.

Baada ya Stella kusema vile maaskari wale walienda pembeni kunong?onezana na ilionyesha kuwa wanakubaliana kitu. Kumbe walikuwa wakinong?onezana kuwa watumwe maaskari kadhaa nyumbani kwa Thomas ili wakamkamate Thomas mara moja.

Baada ya kunong?onezana kwa muda askari mmoja kati ya wale maaskari wanne alitoka na kwenda kuwaagiza maaskari watano wafuatane naye kwenda kumkamata Thomas huku yeye akiongoza msafara huo.

Wale maaskari wengine watatu waliobaki waliendelea kumuhoji Stella na hivyo walianza kumuuliza maswali na walimuuliza kuwa je anamfahamu Nancy mke wa Lucas?
Baada ya maaskari wale waliokuwa wakimuhoji Stella kwenda pembeni na kunong?onezana kwa muda, askari mmoja kati ya wale maaskari wanne alitoka na kwenda kuwaagiza maaskari wengine watano wafuatane naye ili kwenda kumkamata Thomas kaka yake Lucas huku askari huyo akiongoza msafara huo. Hivyo jumla ya maaskari 6 walikwenda nyumbani kwa Thomas ili kumkamata.

Wale maaskari wengine watatu waliokuwa wamebaki waliendelea kumuhoji Stella na hivyo walianza kumuuliza maswali, na walimuuliza Stella kuwa je anamfahamu Nancy mke wa Lucas? Stella aliwajibu maaskari wale watatu na kuwaambia kuwa ndio anamfahamu Nancy. Baada ya jibu hilo la Stella, maaskari wale watatu waliokuwa wamebaki na waliokuwa wakimuhoji Stella kwa muda huo walizidi kuwa na shauku ya kutaka kujua Stella amemjuaje Nancy na hivyo walimuuliza Stella kuwa je amemfahamuje Nancy na amemfahamu kwa muda gani? Stella aliwajibu maaskari hao na kuwaambia kuwa anamfahamu Nancy kama mke wa Lucas tu na si vinginevyo hivyo hamjui zaidi, zaidi ya kujua tu kuwa ni mke wa Lucas. Baada ya jibu hilo la Stella, maaskari wale walimuuliza tena Stella na kumwambia kuwa je amewahi kuonana na Nancy uso kwa uso? Stella aliwajibu maaskari hao kuwa yeye hajawahi kumuona Nancy uso kwa uso na amemuona tu huyo Nancy kwenye picha tena baada ya yeye Stella kuanza kuishi na Lucas na hivyo hajui chochote kuhusu mke huyo wa Lucas. Baada ya Stella kuwajibu hivyo maaskari wale, maaskari wale waliendelea kumuuliza Stella kuwa kwahiyo hajawahi kabisa kukutana na Nancy uso kwa uso na wala hajawahi kabisa kumtia machoni na pia hamjui kwa undani zaidi ya kujua tu ni mke wa Lucas? Stella aliwajibu maaskari wale na kuwaambia kuwa ndio.

Maaskari wale walimuuliza tena Stella kuwa je anamfahamu yule mtu aliyewavamia Lucas na mke wake Nancy mpaka kupelekea Nancy kukamatwa?

Baada ya maaskari wale kumuuliza tena Stella kuwa je anamfahamu yule mtu aliyewavamia Lucas na mke wake Nancy mpaka kupelekea Nancy kukamatwa? Stella alinyamaza kimya wala hakuwajibu kitu maaskari wale, na walivyoendelea kumuuliza zaidi aliwajibu na kuwaambia kuwa yeye hajui chochote kuhusu mtu huyo.

Baada ya jibu hilo la Stella, maaskari wale walimwambia Stella kuwa anaanza kuleta ubishi wake tena? Hivyo wanamrudisha tena kwenye chumba cha mateso na akitoka huko atasema tu ukweli yeye mwenyewe au watahakikisha anakuwa maiti. Baada ya maaskari wale kumwambia hivyo Stella, Stella aliwajibu na kuwaambia kuwa wakimpeleka kumtesa tena watakuwa wanamuonea tu lakini ukweli ni kuwa yeye hafahamu chochote kuhusu mtu huyo wanayemuulizia.

Baada ya Stella kusema hivyo maaskari wale walimwambia Stella kuwa hivi anawafanya wao ni wajinga? Sasa leo atasema au watahakikisha anakuwa maiti kwani kwa akili tu ya kawaida ni kuwa yeye na grupu lake hilo la kina Thomas ndio watakuwa walimtuma huyo mtu kumuua Lucas kwa mara ya kwanza na walivyoona imeshindikana na mpango wao haujafanikiwa ndio wakaamua kujaribu kumuua tena Lucas kwa mara ya pili kwa kutumia sumu kali sana ambayo ingechukua maisha yake ndani ya dakika chache tu mara baada ya kula chakula kilichowekwa sumu hiyo, lakini bahati nzuri Lucas hakula chakula hicho. Sasa leo atasema ukweli wote na baada ya maaskari hao kusema hivyo waliita maaskari wengine wawili ili wamnyanyue Stella na kumpeleka chumba cha mateso. Stella alivyoona hivyo aliwaambia maaskari wale kuwa anaomba wasimpeleke tena huko na atawaeleza kila kitu. Baada ya Stella kusema hivyo maaskari wale walimwambia Stella kuwa sasa alivyokuwa hataki kusema ukweli je alikuwa anafikiria nini wakati tangia mwanzo walishamwambia kuwa wanachohitaji kutoka kwake ni ushirikiano wake tu na awaeleze kila kitu na asiwafiche kitu chochote.

Stella aliamua kusema ukweli wote baada ya kufikiria yale mateso aliyopewa mwanzo na hakutaka tena kupata mateso kama yale au zaidi ya yale kwani alijua wakimpeleka tena kwa mara ya pili kwenye chumba kile cha mateso anaweza hata kufa hivyo hakuona tena sababu ya kuficha kitu chochote tena kwani hata angeficha kwasasa isingemsaidia chochote zaidi tu ya kuendelea kupata mateso zaidi.

Baada ya Stella kukubali kusema ukweli wote kwa kuogopa mateso zaidi kutoka kwa maaskari hao waliokuwa wakimuhoji, maaskari hao walimuuliza tena Stella kama alikuwa akimfahamu yule mtu aliyewavamia Lucas na mke wake Nancy mpaka kupelekea Nancy kukamatwa. Baada ya kuulizwa swali hilo, Stella bila ya kusita au kumung?unya maneno aliwajibu maaskari hao na kuwaambia kuwa ndio anamfahamu mtu huyo.

Baada ya jibu hilo la Stella, maaskari hao walimuuliza tena Stella kuwa je mtu huyo anaitwa nani? Stella aliwajibu maaskari hao na kuwaambia kuwa anaitwa David Kituka lakini anajulikana zaidi kama Devi. Baada ya jibu hilo la Stella, maaskari hao walimuuliza tena Stella kuwa je ni nani aliyemtuma huyo Devi kumvamia Lucas na mke wake Nancy? Stella aliwajibu maaskari hao na kuwaambia kuwa ni Thomas ndio alimtuma Devi kuwavamia Lucas na mke wake Nancy.

Baada ya jibu hilo la Stella, maaskari hao walimuuliza tena Stella kuwa kwahiyo Thomas ndio bosi wao kwenye hilo grupu lao? Stella aliwajibu maaskari hao kuwa ndio, Thomas ndio ni bosi wao na ndio kiongozi wao mkuu.

Baada ya jibu hilo la Stella, maaskari hao walimwambia Stella kuwa ushirikiano wake kwenye swala hilo ndio utakaomsaidia kumuokoa yeye asipate adhabu kali zaidi hivyo aendelee kuwaeleza ukweli wote na awajibu maswali yao yote kwa ufasaha mkubwa. Baada ya maaskari hao kumwambia hivyo Stella, walimuuliza tena Stella swali lingine, hivyo walimuuliza Stella kuwa je Thomas anafanya kazi gani hasa hapa mjini? Anafanya kazi ya ofisini au? Stella aliwajibu maaskari hao na kuwaambia kuwa Thomas hafanyi kazi ya ofisini bali naye ni mfanyabiashara kama mdogo wake Lucas. Baada ya Stella kujibu hivyo maaskari hao walimuuliza tena kuwa je anafanya biashara gani hasa?

Stella aliwajibu maaskari hao na kuwaambia kuwa Thomas anafanya biashara ya nguo na vitu vya wanawake kama pochi, vipodozi, viatu, na urembo. Baada ya Stella kujibu hivyo maaskari hao walimuuliza tena Stella kuwa je mbali na biashara hiyo ya nguo na vitu vya wanawake je Thomas anafanya biashara gani nyingine? Stella aliwajibu maaskari hao na kuwaambia kuwa ingawa watu wanajua Thomas ni mfanyabiashara wa vitu hivyo lakini ukweli ni kuwa yeye ni mfanyabiashara wa madawa ya kulevya na pia hiyo biashara ya nguo na vitu vya wanawake anaitumia tu kujifichia humo.

Baada ya jibu hilo la Stella, maaskari hao waliendelea kumuuliza maswali Stella na hivyo walimuuliza tena kuwa je na yeye Stella yupo kwenye biashara hiyo? Stella alisita kidogo kujibu swali hilo na alivyokuwa akisita askari mmoja kati ya wale maaskari watatu alimpiga kibao cha nguvu kilichopelekea Stella kuona nyota na giza totoro kwa muda, na wakati askari huyo akimpiga kibao Stella, askari huyo alikuwa amefura kwa hasira na alimwambia Stella kuwa hapo hawapo kucheza hivyo ajibu swali hilo aliloulizwa kabla uvumilivu haujawashinda na kuamua kuchukua hatua kali zaidi.

Baada ya kupigwa kibao hicho na askari yule, Stella aliogopa sana na alijua kuwa asiposema ukweli atapelekwa tena kwenye chumba cha mateso kitu ambacho hakutaka tena kimfike, hivyo baada ya ile hali ya nyota nyota na giza nene kuisha ingawa alikuwa bado na maumivu ya kichwa baada ya kupigwa kibao hicho Stella aliwajibu maaskari hao na kusema kuwa ndio na yeye yumo kwenye biashara hiyo.

Baada ya Stella kujibu hivyo, maaskari hao walimuuliza tena Stella kuwa je kwenye biashara hiyo yeye yupo kama nani yani anafanya kazi gani? Stella aliwajibu na kuwaambia maaskari wale kuwa yeye yupo kama punda,-yaani anabeba madawa hayo ya kulevya kupeleka sehemu mbali mbali ndani ya nchi na nje ya nchi. Baada ya jibu hilo la Stella, maaskari hao walimuuliza Stella kuwa kwahiyo na yeye ameshawahi kubeba mzigo? Stella alijibu ndio ameshawahi kubeba mzigo.

Baada ya jibu hilo la Stella, maaskari hao walimuuliza tena Stella kuwa je huwa anakwenda kwenye nchi gani kuzipeleka au kuzichukua hizo dawa za kulevya? Stella aliwajibu maaskari hao na kuwaambia kuwa alikuwa anakwenda Afrika Kusini, Pakistani, China, Dubai na Brazil ingawa kwasasa hajasafiri kwa muda mrefu tangu aanze kuishi na Lucas.

Baada ya jibu hilo la Stella, maaskari wale walimwambia Stella kuwa ingawa awali alisema kuwa hamjui Nancy mke wa Lucas kwa kumuona kwa macho bali anamjua kwa kumuona tu kwenye picha tena baada ya yeye Stella kuanza kuishi na Lucas, sasa awaeleze ukweli je na Nancy naye pia yupo kwenye hilo grupu lao?
SEHEMU YS KUMI NA NNE 14

Comments