Sehemu ya - 15
Baada ya Lucas kumaliza kuongea na mke wa Thomas, aliamua kwenda kulala muda huo huo huku akiwa na mawazo mengi sana kichwani mwake. Alivyokuwa kitandani ilimchukua muda mrefu sana kupata usingizi kwani alikuwa akiwaza mambo mengi sana bila kupata majibu na kwa muda alimsahau kabisa Stella na alikuwa akimuwazia kaka yake Thomas huku akifikiria sababu hasa iliyofanya kaka yake huyo kukamatwa na mapolisi kama jambazi. Pia Lucas alikuwa akifikiria ni nani huyo anayewafatafata yeye na kaka yake Thomas na pia sababu ya huyo mtu ni nini hasa mpaka kuwafanyia mambo yote hayo!? Lucas aliendelea kuwaza mwishowe alipitiwa na usingizi.
Lucas alikuja kushtuka saa kumi na mbili asubuhi hivyo alikurupuka kutoka kitandani na kuanza kujiandaa, na ilivyofika saa moja na nusu alianza kuondoka kuelekea nyumbani kwa kaka yake Thomas.
Lucas alivyofika nyumbani kwa kaka yake huyo alimkuta Mary mke wa kaka yake Thomas akiwa tayari ameshajiandaa ili waweze kwenda huko polisi. Mary alionyesha akiwa ni mnyonge na mchovu mno na pia macho yake yalikuwa yamevimba sana kuonyesha kuwa alikuwa akilia usiku kucha na kuna dalili zote kuwa hakulala. Lucas alimsalimia shemeji yake huyo na bila ya kupoteza muda alimwambia waondoke kuelekea huko polisi ili wakajue kinachoendelea.
Lucas akiwa njiani na shemeji yake huku yeye akiendesha gari, mara simu yake iliita na alivyoipokea ilikuwa ikitoka polisi na alielezwa kuwa anahitajika huko polisi haraka sana ili kumfahamisha mambo machache kuhusu kesi yake na pia kuna maswali ambayo wangependa kupata ufafanuzi kutoka kwake yeye Lucas mwenyewe. Lucas alijibu na kusema kuwa yuko njiani kwenda huko huko polisi kwani amesikia kuwa kaka yake Thomas amekamatwa. Baada ya Lucas kusema hivyo polisi huyo aliyempigia simu alimwambia kuwa kabla hajaenda kufatilia mambo ya kaka yake huyo inabidi kwanza afike ofisini kwao haraka na baada ya kupewa maelekezo hayo Lucas alikubali na kusema sawa na kuendesha gari mpaka polisi.
Walivyofika polisi, Lucas alimwambia shemeji yake Mary kuwa aende kwanza huko mahabusu alikokuwa Thomas kuona kama kuna uwezekano wowote wa kumuona na kusikilizwa kuhusu dhamana wakati yeye akielekea kwanza huko ofisini alikoitwa na akimalizana nao atakuja kuungana naye ili kuona kama kuna uwezekano wa kupata dhamana kwa ajili ya kaka yake huyo.
Baada ya kumueleza hivyo shemeji yake Mary, Lucas alielekea ofisini kwa maaskari alikoitwa, na alivyofika alikaribishwa na bila kupoteza muda mazungumzo yao yalianza na siku hiyo aliwakuta maaskari wanne, wawili ni wale waliokuja nyumbani kwake siku ya kwanza baada ya kugundua kuwa chakula chake kinaweza kuwa kimewekwa sumu na wengine wawili walikuwa ni maaskari upelelezi Gabriel na Saidi ambao walikuwa wakishughulikia kesi yake ya mwanzo ya kuvamiwa na mtu waliyekuwa wamempa lifti yeye na mke wake Nancy.
Maaskari wale walianza kumwambia Lucas kuwa mwanamke aliyekuwa akiishi naye yaani Stella ni mtu hatari sana tena sana na pia alikuwa akifanya biashara ya madawa ya kulevya na ni mzoefu hasa wa biashara hiyo kwani alikuwa akiyasafirisha madawa hayo ya kulevya bila ya kukamatwa na pia alikuwa akiyasafirisha kwenda nchi mbalimbali kama Afrika Kusini, Pakistani, China, Dubai na Brazil. Je yeye Lucas kwa muda wote aliokuwa naye na kuishi naye anajua lolote kuhusu hilo au alihisi chochote kuhusu hilo?
Baada ya Lucas kuambiwa na maaskari hao wanne kuwa mwanamke aliyekuwa akiishi naye yaani Stella ni mtu hatari sana tena sana na pia alikuwa akifanya biashara ya madawa ya kulevya na kuyasafirisha kwenda nchi mbalimbali kama Afrika Kusini, Pakistani, China, Dubai na Brazil, Lucas alishtuka sana na hakutegemea kabisa kusikia habari hizo kuhusu Stella. Yeye alichokuwa akihisi ni kuwa Stella alimwekea sumu kwenye chakula chake ili kumuua labda kwasababu ya mali alizonazo hivyo labda alifikiri kuwa akimuua ataweza kuchukua hizo mali kwa urahisi au pia inawezekana Stella alitaka kumuua kwasababu labda alitumwa na wafanyabiashara wenzake wasiompenda ambao walikuwa wakiona labda yeye ni tishio kwao kibiashara hivyo ndio maana walitaka kumuua ili apotee kabisa hapa duniani na wao wafanye biashara zao bila ushindani wowote kutoka kwake, lakini hata siku moja Lucas hakuwahi kuwaza kuwa Stella anaweza kuwa anajishughulisha na biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya.
Lucas alibaki ameinamisha kichwa chake chini huku akiwa na mawazo mengi sana. Alianza kujutia uamuzi wake wa kuamua kuishi na Stella na alijilaumu sana tena sana alivyoanza kumpenda Stella na mpaka kufikia hatua ya kutaka kumfanya kuwa mke wake ili tu amsahau mke wake Nancy kwa haraka.
Wakati Lucas akiendelea kuwaza yote hayo, mara alishtuliwa na mmoja kati ya maaskari wale wanne ambaye alimwambia kuwa mbona yupo kimya? Wanahitaji kusikia jibu lake kuhusu swali walilomuuliza kama yeye Lucas kwa muda wote huo aliokuwa akiishi na Stella anajua lolote kuhusu Stella kuwa mtu wa hatari na anayejishughulisha na biashara hiyo haramu au alihisi chochote kuhusu hilo?
Lucas aligutuka kutoka kwenye dimbwi la mawazo alilokuwa amezama na hivyo aliwajibu maaskari wale na kuwaambia kuwa yeye hajui chochote kuhusu hilo na alichokuwa akijua ni kwamba Stella alikuwa ni mwanamke tu wa kawaida kama walivyo wanawake wengine na pia Stella alikuwa akifanya biashara zake ambapo alikuwa akiuza duka la vyombo vya nyumbani mpaka pale yeye mwenyewe Lucas alivyomwambia kuwa aachane na hiyo biashara kwasababu alikuwa akilalamika kuwa hapati faida yoyote na hivyo yeye alimwambia kuwa atampa mtaji wa kufanya biashara nyingine au kama atapenda basi amsaidie huko kwenye kampuni yake. Na wakati akisubiria ili ampe mtaji wa kuanzisha biashara nyingine atakayoipenda au kama atapenda aende kufanya kazi kwenye kampuni yake, Stella alikuwa akikaa tu nyumbani na wala yeye hakuona hali yoyote kuashiria kuwa labda kuna vitu anavifanya na pia isitoshe tangu waanze kuwa pamoja hajawahi kumuona akisafiri kwenda popote ingawa aliwahi kumuelezaga kuwa vyombo vyake alivyokuwa anaviuza alikuwa akivifata yeye mwenyewe nje ya nchi, ndio maana yeye Lucas anashangaa sana hiyo biashara ya madawa ya kulevya alikuwa akiifanya saa ngapi!? na alikuwa akiyasafirisha hayo madawa wakati gani?
Baada ya Lucas kusema hivyo, maaskari wale walimwambia Lucas kuwa tangu Stella aanze kuishi na yeye Lucas hajasafiri tena na alipumzika kufanya hiyo biashara ya madawa ya kulevya tangu aanze kuishi na yeye Lucas, kwani kazi yake ilikuwa ni moja tu yaani kummaliza yeye Lucas. Na baada ya maaskari wale kusema vile, kabla Lucas hajasema kitu chochote maaskari wale walimwambia Lucas kuwa na ripoti ya majibu yaliyopatikana kutoka kwa mkemia mkuu baada ya kukichunguza chakula hicho inasema kuwa chakula kile kilikuwa na sumu, tena sumu hiyo iliyowekwa kwenye chakula hicho ilikuwa ni sumu kali sana ambayo ina uwezo wa kumuua mwanadamu ndani ya dakika kadhaa yani hata dakika ishirini hazifiki hivyo kama yeye Lucas angekula chakula hicho hata kijiko kimoja tu sasa hivi wasingekuwa naye tena. Na ndio maana chakula hicho kilibadilika rangi muda mfupi baada ya kuwekwa sumu hiyo kuonyesha kuwa sumu hiyo tayari ilikuwa imeshaanza kufanya kazi, na kwasababu yeye Lucas hakula chakula hicho ndani ya muda huo mfupi tangia sumu hiyo iwekwe ndio maana alikuta tayari chakula kimeshabadilika rangi kuonyesha kuwa sumu hiyo tayari ilikuwa imeshaanza kufanya kazi na ilikuwa ikiendelea kufanya kazi tangu ilivyowekwa. Na pia mtu angekula chakula hicho chenye sumu hiyo hata angepewa tiba gani uwezekano wa kupona ulikuwa haupo kabisa labda kama angekuwa ni malaika aliyeshushwa kutoka mbinguni.
Baada ya maaskari hao kumwambia hivyo Lucas, wala hawakusubiri Lucas aseme kitu chochote na mmoja kati ya maaskari wale alimwambia Lucas kuwa na kama alikuwa hafahamu ni kwamba huyo Stella anamjua vizuri sana mtu aliyewavamia siku ile yeye aliyoenda kazini kwa mke wake Nancy kumchukua. Baada ya maaskari hao kusema hivyo, Lucas alishika kichwa chake kwa mshangao mkubwa sana na alisema kuwa ?Kwahiyo Stella na Nancy wanajuana!!??
Baada ya Lucas kusikia kuwa Stella anamfahamu vizuri sana mtu aliyewavamia yeye na mke wake Nancy siku aliyokwenda kazini kwa mke wake huyo kumchukua na hivyo kupelekea yeye kushika kichwa chake kwa mshangao mkubwa sana na kusema kuwa ?Kwahiyo Stella na Nancy wanajuana!!?? maaskari wale walimuuliza Lucas kuwa kwanini anafikiria Stella na mke wake Nancy wanajuana? Lucas alijibu na kuwaambia maaskari hao kuwa amefikiria hivyo kwasababu mke wake huyo kwasasa ndio anayeshikiliwa na yuko polisi kwa kumtafuta yule mtu ili amuue yeye, sasa kama Stella anamfahamu vizuri huyo mtu maana yake Stella na mke wake Nancy watakuwa wanajuana vizuri sana na ukute Stella alikuja kwenye maisha yake ili kufanikisha hilo lengo la Nancy la kutaka kumuua baada ya jaribio lake la kwanza kushindwa.
Baada ya Lucas kusema hivyo, maaskari hao walimwambia Lucas kuwa imegundulika kuwa mke wake Nancy wala hahusiki kabisa na chochote kuhusu wao kuvamiwa siku ile yeye Lucas aliyokwenda kumchukua mke wake huyo na pia mke wake huyo wala hamjui Stella kabisa na wala hajawahi kumuona.
Baada ya maaskari kumwambia hivyo Lucas, Lucas aliwauliza maaskari hao kwa mshangao kuwa sasa kama mke wake Nancy hahusiki kabisa je huyo mtu alijuaje kama yeye anakwenda kazini kwa mke wake siku hiyo mpaka naye akaenda huko na kama mke wake hahusiki mbona alimkuta huyo mtu anaongea na mke wake wakati mke wake huyo akimsubiri? Na pia kama mke wake hahusiki je ni nani basi anayehusika!?
Baada ya maswali hayo ya Lucas, maaskari walimwambia Lucas kuwa imejulikana kuwa yeye mwenyewe Lucas ndio alimwambia mtu kuwa anakwenda kazini kwa mke wake kumchukua hivyo akumbuke vizuri alimwambia nani? Ingawa siku ile walivyomuhoji alikataa na kusema kuwa hakumuaga wala kumwambia mtu yeyote kuwa anakwenda kazini kwa mke wake huyo.
Baada ya maaskari hao kusema hivyo, Lucas alishangaa sana na kusema ?mimi!?? na maaskari wale walimwambia ndio yeye hivyo ajaribu kukumbuka vizuri alimwambia nani kuwa anakwenda kumchukua mke wake kazini kwake. Lucas alifikiri sana na mwishowe aliwajibu maaskari wale na kuwaambia kuwa kwa kweli wala hakumbuki kabisa kama alimuaga au kumwambia mtu yeyote kuwa anakwenda kazini kwa mke wake siku ile.
Baada ya jibu hilo la Lucas maaskari wale walimwambia Lucas kuwa basi kama alikuwa hafahamu ni kwamba pale kazini kwake kuna mtu amepandikizwa ambaye ndio huwa anatoa information zote jinsi mambo yanavyokwenda hapo kazini kwake, yani huyo mtu ndio anatoa habari zote kuhusu kila kitu kama vile nani kaingia na nani ametoka hapo kazini kwake. -Baada ya Lucas kuambiwa hivyo alichoka kabisa na alishusha pumzi kwa nguvu na aliuliza je ni nani huyo!? Mbona hajawahi kuwaza wala kufikiria kuhusu hilo hata siku moja kwani kila mfanyakazi pale kazini kwake anafanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa sana na hakuna hali yoyote inayoonyesha kama kuna mtu yeyote anayetaka kumfanyia mabaya! Na hata wao wenyewe maaskari walivyochunguza mawasiliano ya hao wafanyakazi wake na mambo mengine hawakugundua wala kuona hali yoyote inayoweza kuonyesha kuwa kuna wafanyakazi wanaomzunguka.
Baada ya Lucas kuwahakikishia maaskari wale kuwa hakumbuki kabisa kama aliongea na mtu yeyote siku ile aliyokwenda kumchukua mke wake kazini kwake, maaskari wale walimwambia Lucas kuwa je hakumbuki kama aliongea na mmoja wa walinzi wake wanaolinda pale katika ofisi zake!?
Lucas alijitahidi kufikiri na mwishowe alisema ?aahaa nimekumbuka sasa? na baada ya kusema hivyo, maaskari wale walimuuliza Lucas kuwa je amekumbuka nini? Lucas aliwaambia maaskari kuwa amekumbuka kuwa siku ile alivyokuwa anatoka kwenda kumchukua mke wake Nancy kazini kwake aliwakuta walinzi wake wawili wakiwa getini kama kawaida yao wakiendelea kulinda, na walisalimiana, na baada ya kusalimiana, mlinzi wake mmoja akamuuliza kuwa ?Bosi mbona mapema leo!? Au unaenda kupata moja moto na moja baridi?? Lucas aliendelea kuwaambia maaskari wale kuwa wala hakushangaa kuulizwa swali hilo na mlinzi huyo kwani mara nyingi huwa anatoka kazini kwake saa kumi na mbili jioni hivyo kutoka muda ule aliotoka wa saa kumi jioni haikuwa kawaida yake.
Baada ya Lucas kusema hivyo maaskari wale walimuuliza Lucas kuwa baada ya kuulizwa hivyo na mlinzi huyo yeye alimjibu nini!? Lucas aliwaambia maaskari hao kuwa alimjibu mlinzi huyo na kumwambia kuwa anawahi kwenda kumchukua mke wake kazini kwake na wala hakumwambia zaidi kwanini anakwenda kumchukua mke wake na huyo mlinzi naye wala hakumuuliza kwanini ameamua kwenda kumchukua mke wake siku hiyo wakati mke wake huyo naye alikuwa na usafiri wake na alikuwa akijiendesha mwenyewe.
Baada ya Lucas kuwaambia hivyo maaskari hao, maaskari hao walimuuliza Lucas kuwa je mlinzi wake huyo aliyemuuliza swali hilo anaitwa nani? Lucas alijibu na kusema kuwa anaitwa Salehe.- Maaskari wale walimwambia Lucas kuwa sasa mbona mwanzo aliwakatalia katakata kuwa hakumwambia mtu yeyote kama anakwenda kumchukua mke wake sasa anaona jinsi information ndogo sana ilivyochelewesha upelelezi wa kesi yake hiyo? Kwani angesema tangu mwanzo sasa hivi kesi yake ingekuwa imeshakwisha siku nyingi na wangekua wameshasahau sasa ona kwa kutosema information ndogo tu kulivyosababisha matatizo hayo ya kutaka kuuliwa yazidi kuendelea. Lucas huku akitetemeka kwa hasira kwani hakutegemea kabisa kama mlinzi wake Salehe alikuwa ni mamluki aliyepandikizwa na wabaya wake alijibu na kuwaambia maaskari hao kuwa hakuwaza kabisa kama swali aliloulizwa na mlinzi wake huyo ndio lilisababisha wabaya wake wajue anakwenda wapi na pia isitoshe yeye na huyo mlinzi wake Salehe wamekuwa wakitaniana sana, yeye huwa anapenda kumuita afande kwasababu mlinzi huyo kila akimuona huwa anampigia saluti na kumuita Bosi na yeye huwa anacheka kwa utani wake huo na hivyo anamuita afande, hivyo hata alivyomuuliza swali hilo alijua ni sehemu tu ya utani wake na si vinginevyo kabisa. Baada ya kujibu hivyo, maaskari wale walimuuliza Lucas kuwa je kwasasa huyo mlinzi wake bado yupo kazini kwake? Lucas aliwajibu na kuwaambia kuwa ndio mlinzi huyo bado yupo kazini ila siku ya leo ataingia zamu ya usiku.- Baada ya jibu hilo la Lucas, maaskari wale walimwambia Lucas kuwa huyo mlinzi wake wameshamkamata tangia jana usiku na kwasasa yupo hapo kituoni wanamshikilia. Baada ya Lucas kuambiwa hivyo na maaskari wale aliishiwa nguvu kabisa na alibaki kujiuliza maswali mengi na mwishowe aliwauliza maaskari wale kuwa je ni nani aliyemtuma huyo mlinzi na Stella ili wamuue!? Na pia kama huyo mlinzi ndio aliyewaambia wabaya wake kuwa anakwenda kazini kwa mke wake imekuaje sasa wabaya wake wakawahi kufika huko kazini kwa mke wake na pia walimjuaje mke wake!? Baada ya Lucas kusema hivyo maaskari wale walimwambia Lucas kuwa asiwe na wasiwasi kwani maswali yake yote hayo yatajibiwa na pia isitoshe hata mtu aliyetaka kumuua leo atamjua hivyo ngoja wamuwekee hiyo kaseti waliyomrekodi huyo Stella mwanamke aliyekuwa akiishi naye na ambaye alitaka kumuoa ndio atasikia kila kitu na kujua kila kitu na kitendawili kilichomtesa yeye na hata wao maaskari kwa muda mrefu atakitegua leo.
Baada ya maaskari kumwambia Lucas kuwa asiwe na wasiwasi kwani maswali yake yote hayo aliyokuwa nayo yatajibiwa na pia isitoshe hata mtu aliyetaka kumuua leo atamjua walimuwekea Lucas kaseti ya mahojiano kati yao na Stella na kumwambia Lucas aisikilize kwa makini.
Lucas alianza kusikiliza mahojiano hayo kati ya Stella na maaskari hao, mwanzo aliona ni maswali tu ya kawaida hasa maswali waliyokuwa wakimuuliza Stella kama ana husika au ahusiki na kuweka sumu kwenye chakula na jinsi Stella alivyokutana na yeye Lucas, na pia kazi aliyokuwa akifanya Stella kabla na baada ya kukutana na yeye Lucas na mambo mengine. Pia Lucas alikuwa akizidi kushikwa na hasira hasa pale wakati Stella alivyokuwa akisisitiza kuwa alikuwa akiweka chumvi kwenye chakula kile na alivyokuwa akijikanyaga kanyaga kujibu kuwa mara hakuingia jikoni siku ile, mara hiyo ilikuwa ni siku nyingine n.k
Lucas alikaa vizuri na kuanza kusikiliza kwa makini mahojiano hayo hasa pale maaskari hao walivyoanza kumuuliza Stella kuwa kwanini alitaka kumuua Lucas kwa kumuwekea sumu kwenye chakula?
Baada ya kusikia swali hilo, Lucas alikaa vizuri na alianza kusikiliza kwa makini zaidi. Na aliendelea kusikiliza mahojiano hayo kwa umakini zaidi hasa pale Stella alivyojibu kuwa alifanya vile kwasababu alikuwa ametumwa kufanya vile na haukuwa uamuzi wake kufanya vile.
Baada ya jibu hilo la Stella, moyo wa Lucas ulipiga paa na alikuwa anataka tu kusikia jibu la Stella ni nani huyo aliyemtuma kumuwekea sumu kwenye chakula chake na si vinginevyo. Hivyo Lucas aliendelea kusikiliza kwa umakini kabisa mahojiano hayo kati ya Stella na maaskari hao waliokuwa wakishughulikia kesi zake hizo mbili.
Lucas aliendelea kusikiliza jinsi maaskari hao walivyomuuliza Stella kuwa je ni nani huyo aliyemtuma kufanya hivyo? Huku moyo wa Lucas ukidunda kwa nguvu ili asikie ni nani huyo aliyemtuma Stella kumwekea sumu kwenye chakula chake, hakuamini masikio yake pale Stella alivyojibu na kusema kuwa ni Thomas. Hivyo pale pale huku Lucas akiwa amechanganyikiwa na wala akiwa haelewi tena aliwauliza maaskari hao kuwa huyo Thomas aliyemtaja hapo ni nani!? Ni Thomas gani?
Maaskari hao walimwambia Lucas kuwa yeye ni mwanaume sasa mbona ana panic hivyo? Hivyo avute subira na aendelee kusikiliza hayo mahojiano yeye mwenyewe kwa masikio yake kwani hata hilo swali lake analowauliza sasa litajibiwa pia.
Baada ya kuambiwa hivyo na maaskari hao, Lucas alikuwa akijiuliza maswali mengi sana kichwani mwake, je huyo Thomas ni nani!? Usikute huyo Stella anataka kumbambikizia kesi kaka yake ili awavuruge wao kama familia ili kumkomoa yeye Lucas wakati mtu aliyemtuma amemficha na hajamtaja. Na baada ya kuwaza hivyo Lucas alisema kamwe hatakubali kabisa hilo litokee eti mtu baki aje awavuruge kwa maneno ya uongo na ya ujinga.
Baada ya Lucas ku panic na kuchanganyikiwa baada ya kusikia Stella akisema kuwa alitumwa na Thomas, maaskari hao walimwambia Lucas atulie ili aendelee kusikiliza mahojiano hayo, hivyo Lucas alitulia ingawa alikuwa bado hajawa vizuri, na maaskari hao walibonyeza tena kaseti hiyo ili mahojiano kati yao na Stella yaendelee kusikika, maana walisimamisha kwa muda baada ya kuona Lucas amechanganyikiwa baada ya kusikia jina la kaka yake Thomas likitajwa na Stella kama ndio mtu aliyemtuma kumuwekea sumu Lucas na hivyo Lucas akawa hasikilizi tena mahojiano hayo.
Mahojiano yaliendelea na hatimaye ilifika sehemu ambapo maaskari wale walimuuliza Stella kuwa huyo Thomas ni nani? na yeye akajibu kuwa Thomas ni kaka yake na Lucas.- Na alivyoulizwa ni kaka yake Lucas kivipi? Ni binamu yake? au ni mtoto wa shangazi yake au mjomba wake? au ni mtoto wa mama yake mkubwa au mama yake mdogo? Stella naye alijibu kuwa ni kaka yake wa damu na Lucas yaani ni baba mmoja mama mmoja na wamezaliwa wawili tu, wa kwanza akiwa ni Thomas kwa kuzaliwa- na wa pili ambaye pia ni wa mwisho ni Lucas.
Baada ya jibu hilo la Stella, Lucas alisimama na alianza kusema kuwa haiwezekani kabisa kaka yake Thomas akamfanyia hivyo, huyo mwanamke ni muongo mkubwa na anataka kuisambaratisha familia yao. Pia Lucas aliwageukia maaskari wale na kuwaambia kuwa hivi wanaamini vipi ujinga kama huu!? Yani na wao wanauamini huu upumbavu aliowaeleza huyu mwanamke muuaji ili kuiharibu familia yao!?
Pia Lucas huku akiendelea kukataa na kusema kuwa huyo mwanamke ni muongo, aliendelea kusema kuwa kwanza huyo Stella na kaka yake Thomas wamejuana kupitia yeye sasa huyo Thomas atamtumaje tena huyo Stella kufanya kitu kama hicho wakati walikuwa hata hawajuani na wala hawana ukaribu wowote? Hivyo huyo Stella atafute tu mbinu nyingine ya kuwavuruga na si hiyo kwani kwa hilo amegonga mwamba.
Baada ya Lucas kusema maneno hayo huku akiwa na hasira, maaskari wale walimwambia Lucas kuwa hebu akae chini kwanza na ajikaze na atulie. Wanaelewa kabisa hali aliyokuwa nayo kwasasa, na pia isitoshe kwa vyoyote vile ni lazima iwe ngumu sana kuamini, hivyo atulie kwanza amalizie kusikiliza mahojiano yote ndio wataendelea na mambo mengine, pia isitoshe bado wako kwenye uchunguzi hivyo ukweli utajulikana tu kama ni kweli kaka yake huyo alitaka kumuua kama alivyoeleza Stella ama la.
Lucas alijitahidi kujikaza na kukaa chini kwenye kiti huku akiwaza na kujiuliza kuwa hivi hawa maaskari mbona ni wapuuzi kiasi hiki!? Wanaaminije uongo unaosemwa na huyu mwanamke muuaji!? Hivi huyu mwanamke anajua umuhimu wa familia kweli!? Hivi huyu shetani Stella ana familia kweli mpaka anataka kuivuruga familia yao kiasi hiki!? Lucas aliendelea kujilaumu kuwa amejiingiza kwenye balaa gani hili kwa kujaribu kumpenda huyo Stella ili amsahau mke wake Nancy?- Lucas alikuwa akiona kama anaota vile yani alikuwa bado haamini kabisa kinachoendelea hapo na alichokisikia. Alitamani sana iwe ni ndoto na aamke kutoka usingizini na akute kuwa ilikuwa ni ndoto tu na sio kweli.
Pale pale Lucas akakumbuka kuwa ndio maana kaka yake Thomas amekamatwa! Kumbe kwasababu ya uongo wa huyu mwanamke Stella! Ila kwa hili hatakubali kamwe na atahakikisha anapigana kiume mpaka Stella anamtaja huyo mtu aliyemtuma na sio kaka yake Thomas.- Baada ya Lucas kuwaza hivyo huku akiwa bado na uchungu na huzuni ikiwa imetawala uso wake aliwauliza maaskari wale kwa upole kuwa kwahiyo hiyo ndio sababu iliyofanya wamkamate kaka yake Thomas? Maaskari wale walimjibu Lucas na kumwambia kuwa ndio, hiyo ni sababu kubwa iliyofanya wao wamkamate kaka yake huyo, na pia kuna sababu nyingine nyingi zinazofanya wamshikilie ndio maana wanamtaka atulie ili amalize kusikiliza mahojiano yote na ndio waendelee na mambo mengine.
Baada ya jibu hilo la maaskari hao, Lucas alishusha pumzi kwa nguvu na kuegemea kwenye kiti huku akiwa amepoteza matumaini kabisa na akiwa anaomba kimoyo moyo kuwa isiwe kweli bali awe mtu mwingine na si kaka yake Thomas.
Maaskari hao pamoja na Lucas waliendelea kusikiliza mahojiano yale kati ya maaskari hao na Stella ambayo yalikuwa yamerekodiwa, na Lucas alichoka kabisa pale aliposikia Stella akisisitiza kuwa anachosema kuhusu Thomas kaka yake Lucas ndio aliyemtuma kufanya hivyo ni ukweli mtupu kabisa na wala hadanganyi au kumsingizia mtu yeyote.
Pia Lucas alinyong?onyea kabisa pale aliposikia Stella akisema kuwa anamfahamu Nancy kama mke wa Lucas tu na si vinginevyo hivyo hamjui zaidi, zaidi ya kujua tu kuwa ni mke wa Lucas na pia kuwa yeye hajawahi kumuona Nancy uso kwa uso na amemuona tu huyo Nancy kwenye picha tena baada ya yeye Stella kuanza kuishi na Lucas, na hivyo hajui chochote kuhusu mke huyo wa Lucas na pia Nancy hahusiki kwa chochote kile kilichotokea siku ile yeye na Lucas waliyovamiwa na pia Nancy hajui lolote kuhusu mtu yule aliyewavamia, na hamjui kabisa huyo mtu, hivyo yeye ni victim tu.
Baada ya Lucas kusikiliza mahojiano yote kati ya maaskari hao na Stella alibaki amelowa kabisa kwani mambo aliyoyasikia hakuamini kabisa na wala hakutegemea kama yanaweza kufanywa na kaka yake Thomas! Hakuwaza hata siku moja kama Thomas alikuwa anafanya biashara ya madawa ya kulevya na pia alikuwa ni mtu hatari kiasi hicho huku akiongoza kundi la watu hatari sana.
Pia kilichomsikitisha zaidi Lucas ni jinsi kaka yake huyo alivyokuwa hana hata huruma eti alipanga kwanza kumuua yeye halafu angefanikiwa kumuua yeye angekuja kumuua na mke wake kipenzi Nancy, na baada ya kuwaua wote yeye na mke wake Nancy eti alipanga kummaliza mtoto wake Henry kidogo kidogo kwa madawa ya kulevya! na mpaka angekuwa mkubwa mtoto wake huyo angekuwa ni teja hivyo hata asingekuwa na uwezo tena wa kufatilia hizo mali za baba yake yaani za kwake yeye Lucas. -Hiyo sentensi ilimuumiza moyo sana Lucas na aliona ni kama vile mkuki umechoma kwenye moyo wake lakini aliamua kujikaza tu ingawa hata nguvu zilikuwa zimemuishia kwa wakati huo. Tena kibaya zaidi kaka yake huyo alitaka huyo mtu sijui Devi eti ampige yeye Lucas risasi ya kichwa kabisa badala ya begani alikokuwa amempiga! Lucas aliendelea kuwaza na kusema yani mali tu ndio zimemfanya kaka yake huyo ageuke kuwa mnyama kiasi hicho mpaka kutaka kuisambaratisha familia yake yeye Lucas ambaye ni mdogo wake wa damu, bora hata kama labda angekuwa ni ndugu yake wa mbali kidogo!
Lucas alianza kukumbuka jinsi siku ya kwanza alivyomtambulisha Stella kwa kaka yake Thomas huku akimwambia kaka yake huyo kuwa Stella ndio atakuwa mke wake kwasasa na jinsi kaka yake huyo pamoja na Stella walivyokuwa wamejikausha kama vile hawajuani kabisa. Tena Thomas alikuwa akimsifia Stella na kusema kuwa huyo ni mwanamke mzuri na anamfaa kumbe walikuwa wakimchora tu!? Pia Lucas alikumbuka jinsi mwanzo mke wake Nancy alivyokamatwa na kupelekea yeye kukosa raha kwa miezi kadhaa kwa kumuwaza mke wake huyo lakini cha ajabu ni huyo huyo Thomas ndio alikuwa akimwambia kuwa aachane na huyo mwanamke muuaji yaani Nancy na ikiwezekana atafute mwanamke mwingine haraka iwezekanavyo ili kumsahau huyo Nancy na pia ni yeye aliyemwambia kuwa asiende hata huko mahabusu kumuangalia mke wake huyo na amuache tu afie huko jela kwasababu alitaka kumuua yeye Lucas. Pia Lucas aliendelea kukumbuka jinsi ambavyo kaka yake huyo alivyokuwa akimpigia simu mara kwa mara na kumwambia kuwa amsahau huyo Nancy na atafute mwanamke mwingine tena haraka iwezekanavyo na ndipo ilipopelekea yeye akakutana na Stella na kuanzisha mahusiano naye -ili tu amsahau mke wake Nancy, kumbe alikuwa akifanya kosa kubwa sana kwenye maisha yake na wala hakujua kama Thomas- walifanya mipango na huyo Stella ili huyo Stella ajilete kwake. Na baada ya kukumbuka hivyo Lucas akainamisha kichwa chake chini na kuanza kulia mpaka maaskari wakamuonea huruma na wakaambiana kuwa wamuache kwanza mpaka hiyo hasira aliyokuwa nayo iishe kwani hapo alipo analia kwasababu atakuwa anajiuliza maswali mengi sana na kukumbuka mambo mengi sana na mpaka ukiona mwanaume analia ujue kweli ameumia sana.
Lucas huku akiwa analia alianza kukumbuka jinsi alivyokutana na Stella, kwani alikutana naye kipindi ambacho alikuwa ni mtu mwenye mawazo sana na aliyekuwa amekata tamaa ya maisha yake. Na siku moja akiwa yupo baa anakunywa bia ili kupoteza mawazo hayo yaliyokuwa yamemsonga sana Stella alikuja kukaa kwenye meza yake na kuanzisha mazungumzo ya hapa na pale mpaka wakaanza kuzoeana, na ingekuwa zamani angejiuliza je huyo Stella alijuaje kama yeye yupo hapo wakati alikuwa hata hamjui!? Lakini sasa jibu analo, kwani lazima itakuwa huyo mlinzi aliyekuwa amepandikizwa na kaka yake Thomas kwenye ofisi zake ndio alimwambia Thomas na Thomas ndio akamtuma huyo Stella mahali hapo kwani hiyo ni sehemu ambayo alikuwa akipenda kwenda mara kwa mara kunywa bia mbili au tatu baada ya kutoka kazini ili kuondoa mawazo tangu yeye na mke wake Nancy wapate matatizo ya kuvamiwa na pia mke wake Nancy akamatwe, na baada ya kunywa hizo bia zake mbili au tatu ndio alikuwa akirudi nyumbani kwake na kufikia kula na kulala. Hivyo ndivyo alivyokutana na Stella na kuanza kuzoeana naye mpaka kufikia hatua ya kuishi pamoja, na kwasababu kaka yake Thomas alikuwa akimwambia mara kwa mara atafute mwanamke mwingine haraka iwezekanavyo ili kumsahau mke wake Nancy, hivyo yeye Thomas ndio alikuwa wa kwanza kumtambulisha kwa Stella na wakati anawatambulisha wala hawakuonyesha kama wanajuana kabisa, -sana sana walivyokuwa wakibaki peke yao yani yeye Lucas na kaka yake Thomas baada ya Stella kutoka kidogo kaka yake huyo alikuwa akimsifia Stella na kusema anafaa kuwa mke wake na ni chaguo zuri.
SEHEMU YA KUMI NA TANO 16

Comments
Post a Comment