Hadithi Lucas 16

Sehemu ya - 16

Lucas aliwaambia maaskari hao kuwa Stella tangu aishi naye kwa kipindi kifupi tu alichokuwa naye amewahi kuwa mjamzito mara mbili na kibaya zaidi mimba zote hizo mbili zilitoka katika mazingira yasioeleweka hivyo inawezekana hazikuwa zinatoka bali alikuwa anazitoa yani sasa ndio anaanza kupata jibu kuhusu zile mimba za Stella zilivyokuwa zinatoka.

Wakati Lucas akiwaambia hivyo maaskari hao, ni kweli kabisa kipindi anakaa na Stella, Stella alishika mimba mara mbili lakini kwasababu Thomas alimpandikiza ili tu aanzishe uhusiano na Lucas na malengo yake yatimie hivyo Stella hakutakiwa kabisa kuwa serious na uhusiano huo kwani hapo kwa Lucas alikuwa kazini, lakini kadri alivyokuwa akikaa na Lucas kidogo kidogo Stella alianza kumpenda Lucas na akawa anamchukulia kama mume wake na sio tena kama mtu ambaye ametumwa amuue. Ingawa Thomas mara kwa mara alikuwa akimsumbua na kumwambia Stella kuwa amemtuma hapo nyumbani kwa Lucas kwa kazi moja tu ila sasa anaona kazi imeanza kumshinda hivyo uvumilivu ukimshinda atamuona mbaya. Na wakati Stella alivyopata mimba ya kwanza, alikwenda kwa Thomas na kumwambia kuwa hapo alipo ana ujauzito na Lucas anafahamu kuwa yeye ni mjamzito kwasasa na pia isitoshe ameanza kumpenda Lucas kwa jinsi anavyo mcare hivyo alikuwa anaomba waachane na hayo mambo ya kumuua na atafute njia nyingine ili kujipatia hizo mali za Lucas na ikiwezekana hata yeye Stella atamsaidia kwa hilo kwani anapenda kumzaa huyo mtoto na pia anapenda Lucas awe mume wake, na baada ya Stella kumwambia hivyo Thomas, Thomas alimwambia Stella kuwa hivi amechanganyikiwa!? Hivi ni mzima kweli huko kichwani kwake!? Pia alimwambia kuwa yeye alimtuma huko kwa Lucas kwa kazi moja tu ya kumuua Lucas na sio kujibebesha mimba hivyo akimletea upuuzi atalifumua hilo tumbo lake kwa bastola muda huo huo. Na kwasababu Stella alikuwa akiujua ukatili wa bosi wao huyo alimuomba msamaha na Thomas alimwambia kuwa hataki kuiona hiyo mimba yake ifikapo kesho saa nane mchana na hivyo Stella alikuwa hana jinsi tena zaidi tu ya kwenda kuitoa hiyo mimba. Na mimba ya pili alivyoipata ilibidi nayo aitoe haraka hata kabla Thomas hajajua kwani alihisi bosi wake huyo anaweza kumuua kabisa safari hii kama akisikia ana mimba nyingine tena.

Wakati Lucas akiwa bado polisi akiendelea kusikiliza mahojiano kati ya Stella na maaskari wale waliokuwa wakimuhoji, kwa wazazi wake Nancy nako walikuwa hawajui kinachoendelea tena huko nyumbani kwa Lucas tangu walivyoambiwa na Rehema mmoja wa wafanyakazi wa Lucas kuwa Stella mwanamke aliyekuwa akiishi na Lucas amekamatwa na Fatuma ameachiwa huru.

Siku hiyo baba yake Nancy akiwa amekaa sebuleni pamoja na Anthony mdogo wake Nancy, huku mama yake Nancy na mdogo wake Nancy msichana yaani Julia wakiwa jikoni wakipika mara simu ya baba yake Nancy iliita na alivyoipokea aliyekua akiongea alijitambulisha kuwa yeye ni polisi na amempigia simu muda huo ili kumjulisha kuwa binti yake Nancy ameachiwa huru na kwasasa yupo hapo kituo cha polisi akimsubiri hivyo aende kumchukua maana hana nauli ya kufika huko nyumbani kwao. Baba yake Nancy hakuamini kile alichokuwa akikisikia na hivyo aliuliza tena kwa mara ya pili kuwa eti anasema mwanae Nancy ameachiwa huru!? Yaani yuko huru!? Yule askari aliyepiga simu alijibu na kusema kuwa ndio kama alivyokuwa amemwambia mwanzo hivyo aende kumfata hapo polisi na baada ya jibu hilo askari yule aliagana na baba yake Nancy, na baba yake Nancy aliweka simu yake juu ya meza na kuweka mikono yake kichwani na kuanza kumuita mama yake Nancy aliyekuwa jikoni kwa sauti ya juu.

Mdogo wake Nancy yaani Anthony ambaye aliyekuwa amekaa sebuleni na baba yake wala hakuelewa kitu na alibaki akimshangaa baba yake huyo huku akijiuliza je kaambiwa nini kwenye simu hiyo aliyopigiwa muda si mrefu!? Je ni habari nzuri au ni habari mbaya? Wakati baba yake Nancy akiendelea kumuita mama yake Nancy kwa nguvu huku Anthony akishangaa, mama yake Nancy aliyekuwa jikoni na Julia walikuja sebuleni wote kwa pamoja huku wakikimbia kwani hawakujua mzee huyo amepatwa na kitu gani.

Mama yake Nancy na Julia mdogo wake Nancy walivyofika sebuleni, walimkuta baba yake Nancy akiwa amesimama huku akiendelea kumuita mke wake huyo. Baba yake Nancy alivyomuona tu mke wake huyo na binti yake Julia wakiwa wamefika mahali hapo alimrukia mke wake huyo na huku machozi ya furaha yakimtoka alianza kumwambia mke wake huyo kuwa Mungu amesikia maombi yao. Huku Julia na Anthony wakiendelea kushangaa kwasababu walikuwa hawajui kinachoendelea, mama yake Nancy alimwambia mume wake huyo kuwa mbona hamuelewi? basi anaomba atulie na amwambie Mungu amejibu maombi yao kivipi? Baada ya swali hilo la mama yake Nancy, baba yake Nancy alisema maneno matatu tu kuwa ?Nancy yuko huru? na baada ya kusema hivyo alikaa tena kwenye kochi na kuinamisha kichwa chake chini huku akifuta machozi ya furaha yaliyokuwa yakitiririka machoni mwake.

Baada ya baba yake Nancy kusema kuwa Nancy yuko huru, mama yake Nancy alipatwa na mshangao kwa dakika kadhaa halafu huku akiwa bado anaona kama vile anaota na kile alichokisikia kutoka kwa mume wake huyo ni ndoto alimsogelea mume wake huyo ambaye alikuwa amekaa kwenye kochi kwa muda huo huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini na akifuta machozi yaliyokuwa yakimtiririka na kumshika bega lake la kulia na kumuuliza tena hivi amemwambiaje!? Baba yake Nancy alimjibu mama yake Nancy na kumwambia kuwa amesema kuwa ?Nancy yuko huru?. Baada ya jibu hilo la baba yake Nancy, mama yake Nancy alimuuliza baba yake Nancy kuwa amejuaje kama Nancy yuko huru wakati muda wote huo alikuwa yupo hapo sebuleni akiangalia Televisheni na wala hajatoka nje kabisa leo, au anaota? Baba yake Nancy alimjibu mama yake Nancy na kumwambia kuwa wala haoti na anachomwambia ni ukweli mtupu kwani amepigiwa simu na askari mmoja wa kike muda sio mrefu akiwa hapo hapo sebuleni na mtoto wao Anthony ni shahidi, na askari huyo amemwambia kuwa Nancy ameachiwa huru hivyo anatakiwa akamchukue huko polisi kwani hana nauli ya kufika hapo nyumbani.

Baada ya baba yake Nancy kusema hivyo, mama yake Nancy alimgeukia Anthony na kumuuliza kuwa eti ni kweli anayosema baba yake? Anthony alimjibu mama yake na kumwambia kuwa ni kweli baba yake amepigiwa simu muda si mrefu wakiwa hapo hapo sebuleni kabla hajawaita wao lakini alichoongea kwenye simu yeye hafahamu kwani alikuwa hasikilizi mazungumzo yao. Baada ya jibu hilo, mama yake Nancy alimwangalia tena mume wake huyo na kumuuliza kwahiyo anachosema ni ukweli? Baba yake Nancy alijibu na kusema kuwa ndio ni ukweli na ameambiwa Nancy anamsubiri huko polisi hivyo inabidi afanye haraka kwenda kumchukua ili mwanae huyo asichoke kumsubiri.

Baada ya jibu hilo la baba yake Nancy, mama yake Nancy alianza kulia kwa sauti huku akiruka ruka na kusema kweli Mungu amewasikia maombi yao na pia Anthony na Julia nao waliungana na wazazi wao kufurahia huku wote kwa pamoja wakitoa machozi ya furaha. Baada ya kufurahi kwa dakika kadhaa baba yake Nancy alisema ngoja yeye awahi kwenda huko kituo cha polisi ili awahi kwenda kumchukua mwanae huyo. Baada ya baba yake Nancy kusema hivyo mama yake Nancy na wadogo zake Nancy, Julia na Anthony nao wote kwa pamoja walisema kuwa wanakwenda nao pia kumfata dada yao huyo kwani hawaamni kabisa kama kweli yupo huru mpaka pale watakavyomuona wenyewe kwa macho yao, na baada ya kila mtu kusema anataka kwenda huko polisi kumchukua Nancy, walikubaliana kuwa waende wote na baba yake Nancy alimpigia simu dereva wa taxi ambaye huwa wanamtumia mara kwa mara wakiwa na dharura na ambaye hata akiwa hana pesa huwa anamtumia halafu anakuja kumlipa baadaye. Hivyo baada ya dakika kadhaa kupita tangu baba yake Nancy ampigie simu dereva huyo, dereva huyo alifika nyumbani kwa kina Nancy na familia hiyo ya Nancy walifunga nyumba na kuondoka kwenda polisi.

Familia ya Nancy walivyofika polisi hawakuamini pale walipomuona Nancy akiwa amesimama na mfuko wake wa rambo akiwasubiri huku akiwa amesimama na askari mmoja wa kike ambaye walikuwa wakiongea.

Nancy alivyowaona ndugu zake hao aliwakimbilia huku machozi yakimtoka, na wazazi wake pamoja na wadogo zake nao walimkimbilia na walivyokutana walirukiana kwa furaha na wote kwa pamoja walianza kulia huku baba yake Nancy akiwa amesimama pembeni akimuangalia mke wake huyo na watoto wake wote watatu wakiwa wameungana tena.

Baada ya muda Nancy na ndugu zake walimuaga askari yule wa kike aliyekuwa amesimama na Nancy pale nje na walianza kuondoka kuelekea kwenye taxi iliyokuwa imewaleta, na wakati wanaondoka kuelekea kwenye taxi iliyokuwa imewaleta mara walimuona Lucas ambaye alikuwa ndio anatoka kwenye ofisi za maaskari alikokuwa anasikiliza mahojiano kati ya Stella na maaskari ambao walikuwa wakishughulikia kesi yake, hivyo Lucas wakati anatoka huku akiwa amechanganyikiwa na akiwa amevua koti na tai alivyokuwa amevivaa na kuvishika mkononi hakuamini macho yake pale alipomwona Nancy akiwa na wazazi wake na wadogo zake Julia na Anthony.

Lucas alivyowaona kina Nancy moyo wake ulilia paa na wala hakujua cha kufanya na alibaki akimwangalia Nancy kwa huzuni na Nancy naye alibaki akimwangalia Lucas kwa huzuni. Ilipita kama dakika 5 hivi Lucas na Nancy wakiangaliana na kila mmoja akiwaza la kwake moyoni mwake, kuona hivyo mama yake Nancy na Julia walimshika Nancy mkono na kumuongoza kwenye ile taxi waliyokuwa wamekuja nayo. Walivyofika kwenye taxi hiyo walipanda huku baba yake Nancy akikaa mbele, na mama yake Nancy na watoto wake wote watatu wakikaa nyuma, na baada ya kupanda kwenye taxi hiyo dereva aliwasha gari na kuondoka mahali hapo huku Lucas akiwa bado haamini kabisa macho yake kama ile taxi imemchukua mke wake kipenzi Nancy. Lucas alitamani sana kama angemchukua yeye -Nancy kwenye gari yake ya kifahari aliyokuwa amekwenda nayo pale polisi na kurudi wote nyumbani kwao lakini matokeo yake mke wake huyo amemuona tu kwa mbali na wala hakupata hata muda wa kusalimiana naye yeye pamoja na wazazi wake na wadogo zake.

Wakati Lucas akiendelea kuishangaa ile taxi iliyokuwa imemchukua mke wake Nancy pamoja na ndugu zake ikiondoka mahali pale, Lucas aligutushwa na sauti ya Mary mke wa Thomas aliyekuwa akimuita ?shemeji shemeji? huku akimwambia kuwa mbona amekaa sana huko alikokuwa amekwenda yani karibia masaa manne yamepita!? Lucas wala hakumjibu Mary mke wa Thomas hilo swali lake na bado aliendelea kuwa mbali sana kimawazo. Ingawa Lucas hakumjibu Mary swali lake hilo alilokuwa amemuuliza, Mary alimwambia tena Lucas kuwa amejaribu kila alivyoweza kumuombea mume wake Thomas dhamana lakini imeshindikana na maaskari wamemkatalia katakata kumpa dhamana labda yeye Lucas akienda wanaweza kumsikiliza kwasababu yeye ni mwanaume. Mary alivyomaliza kumwambia hivyo Lucas alishangaa kuona Lucas wala hamjibu kitu na amenyamaza kimya na alivyomwangalia vizuri zaidi ndio akagundua kuwa hata koti ambalo alikuwa amelivaa alikuwa amelivua na alikuwa amelishikilia mkononi, ingawa mwanzo alidhani labda atakuwa amevua koti hilo kwasababu ya joto lakini alishangaa zaidi alivyoona Lucas amevua mpaka na tai na alikuwa hayupo pale kabisa kimawazo na hata alivyokuwa akimuongelesha inaonekana alikuwa hamuelewi kabisa ndio hapo Mary alimshika Lucas begani na kumwambia kuwa mbona anaonekana yupo mbali sana kimawazo!? Kwani huko ofisini kwa maaskari alikokwenda aliitiwa nini?

Baada ya Mary kumshika Lucas begani na kumwambia kuwa mbona anaonekana yupo mbali sana kimawazo!? Kwani huko ofisini kwa maaskari alikokwenda aliitiwa nini?

Baada ya swali hilo la Mary, Lucas aligeuka na kumwangalia Mary na kumwambia kuwa kwani hajamuona Nancy mke wake hapo maeneo hayo? Mary alishtuka na kumwambia Lucas huku akisema -?Nancy?!? Mbona yeye hajamuona!? Yuko wapi!? Lucas alimjibu Mary na kumwambia kuwa alikuwa maeneo hayo muda si mrefu lakini sasa ameondoka na ndugu zake. Baada ya jibu hilo la Lucas, Mary huku akiwa amepigwa na butwaa na mshangao alimwambia Lucas kuwa ?ameondoka!? Kuelekea wapi!?? Lucas alimjibu Mary na kumwambia kuwa hajui alikokwenda ila ameachiwa huru. Baada ya jibu hilo la Lucas, Mary alimwambia Lucas kuwa na kesi yake iliyokuwa ikimkabili ya kutaka kumuua yeye Lucas nayo vipi!? ?Kwanini wamuachie huru wakati alitaka kumuua!?? Baada ya swali hilo la Mary, Lucas alimwangalia Mary na kumwambia kuwa imeonekana kuwa Nancy hana kosa na sio yeye aliyetaka kumuua ndio maana wamemuachia huru. Baada ya jibu hilo la Lucas, Mary alimuuliza Lucas sasa wamempata muuaji? je ni nani sasa aliyetaka kumuua kama sio huyo Nancy!? Lucas alimwambia Mary kwa kifupi kuwa ni Thomas ndio aliyetaka kumuua.

Baada ya jibu hilo la Lucas, Mary alimuuliza Lucas huyo Thomas ni wa wapi? Ni Thomas gani huyo? Lucas alimwangalia tena Mary na kumwambia kuwa kwani yeye anawajua Thomas wangapi? Baada ya swali hilo la Lucas, Mary kwa mshangao alimwambia Lucas kuwa ina maana anamaanisha ni Thomas mume wake au!? Lucas alimjibu Mary na kumwambia ndio huyo huyo Thomas mume wake.

Mary aliona kama vile anaota au Lucas amechanganyikiwa na pale pale alihisi kuishiwa na nguvu miguuni na hivyo aliamua kukaa chini na aliweka mikono yake kichwani na kuanza kulia huku akimwambia Lucas kuwa ?shemeji huo ni uwongo na sio kweli? na pia aliendelea kusisitiza kuwa mume wake Thomas hawezi kufanya hivyo na pia itakuwa kuna watu wanafanya mipango ya kuwagombanisha tu wao kama ndugu ili wachukiane na iwe faida kwao hao watu, hivi inawezekana vipi kaka yake wa damu atake kumuua yeye mdogo wake wa damu!? Tena maskini ya Mungu wamezaliwa wawili tu, na wanapendana na kujaliana sana.

Baada ya Mary kumwambia hivyo Lucas, Lucas alimwambia Mary kuwa hebu asimchanganye kabisa kwa muda huo kwani kichwa chake hakiko vizuri kabisa, hivyo kama anataka majibu ya maswali yake yote hayo basi aende kumuuliza huyo mume wake muuaji na sio yeye. Na pia kama anaona mume wake hawezi kumfanyia hivyo kwahiyo mke wake Nancy ndio anaweza kumuua si ndio? Maana yeye Mary na mume wake Thomas ndio walikuwa wakimtia maneno yeye Lucas kuwa aachane na huyo Nancy kabisa kwani ni muuaji na ukute alifanya vile kumkodia mtu wa kumuua kwasababu alikuwa anataka mali zake. Sasa leo iweje mke wake yeye yaani Nancy ndio aweze kuwa muuaji na sio huyo mume wake Thomas!?

Baada ya Lucas kusema hivyo huku Mary akiendelea kulia alimwambia Lucas kuwa Nancy anaweza kufanya hivyo yaani kutaka kumuua kwasababu sio ndugu yake bali ni mwanamke tu amemuoa lakini Thomas hawezi kufanya hivyo kwasababu ni ndugu yake wa damu hivyo aliangalie vizuri hilo kwani inawezekana kuna mtego na mchezo wanamchezea ili wamuue kiurahisi kwasababu kaka yake Thomas atakuwa jela hivyo yeye Lucas hatakuwa na msaidizi tena.

Baada ya Mary kusema maneno hayo huku akiendelea kulia Lucas kwa hasira alimwambia Mary kuwa ? Shut up, funga bakuli lako? pia Lucas aliendelea kumwambia Mary kwa hasira kuwa kwani hajui kwa kiasi gani huyo mume wake Thomas na maneno yao wao wote yalivyomuharibia ndoa yake na maisha yake kwa ujumla? na baada ya Lucas kumwambia hivyo Mary, Lucas aliondoka mahali hapo mpaka kwenye gari lake akapanda na kuwasha gari na kuondoka huku akimuacha Mary pale pale alipokuwa amekaa chini baada ya kuhisi kuishiwa nguvu kwenye miguu akiwa bado analia na ameshikwa na butwaa.

Baada ya Lucas kuondoka, Mary hakujua cha kufanya tena kwani alikuwa akiona dunia yote inazunguka kwa wakati huo na pia isitoshe walifika hapo polisi wakiwa wote yeye na Lucas kwa lengo la kuja kuangalia uwezekano wa kumtolea mume wake Thomas dhamana na kufahamu sababu ya kukamatwa kwake lakini matokeo yake huyo shemeji yake yaani Lucas alivyofika hapo aliingia huko maofisini kwa maskari na amekaa huko ofisini karibia masaa manne na alivyotoka ametoka akiwa ni mtu tofauti kabisa huku akiongea mambo yasiyoeleweka kama vile amechanganyikiwa, na kibaya zaidi ameondoka na kumuacha yeye mahali hapo bila hata ya kujua kama ana nauli au hana.

Mary aliendelea kukaa hapo chini kwenye mchanga ili atafakari kwanza yaliyompata na baada ya dakika kadhaa alianza kufikiria je atarudije nyumbani kwake? akaamua kuanza kuangalia kwenye pochi yake kama ana nauli, bahati alikuta akiwa na shilingi elfu 30 hivyo aliamua kuchukua taxi ili imrudishe nyumbani kwake akapumzike kwanza na kutafakari, na alijisemea moyoni kuwa yani akirudi kwa basi anaweza hata kugongwa huko manjiani.

Mary alivyofika nyumbani kwake alimkuta msichana wake wa kazi na watoto wake na alivyowauliza je Henry yupo wapi? Msichana wa kazi alimjibu na kumwambia kuwa Henry amechukuliwa na baba yake kwani baba yake alikuja na amemchukua na kuondoka naye bila hata ya kusema chochote kama atamrudisha lini maana ameondoka na vitu vyake karibia vyote. Baada ya jibu hilo la msichana wa kazi Mary mke wa Thomas alijua kuwa kumbe alivyokuwa anafikiria labda inaweza kuwa sio kweli na pia inawezekana labda Lucas amechanganyikiwa na ndio maana alikuwa akiongea maneno yale yasioeleweka kumbe sivyo na hicho kinachomtokea siku hiyo sio ndoto bali ni kweli kabisa na yote aliyokuwa akiyaongea Lucas alikuwa akiyamaanisha kabisa na hivyo sasa ana kazi ya ziada maana kama mume wake anaitwa muuaji kwasasa tena muuaji eti alitaka kumuua mdogo wake wa damu kweli hilo ni balaa kwenye maisha yake na wala hajui tena itakuaje na ndugu watalipokeaje. Mary aliona kama vile anasikia kizunguzungu hivyo huku akipepesuka na akiwa na uchovu mwingi aliamua kwenda chumbani kwake kwanza kulala na kupumzika kama ataupata hata huo usingizi ili akiamka ndio ajue cha kufanya maana aliona labda akiamka anaweza kukuta sio kweli na hayo mambo yote aliyoambiwa na Lucas kuhusu Thomas yanaweza kuwa sio ukweli na labda ni mambo ya kusingiziwa na uzushi tu usiokuwa na kichwa wala miguu ambao unataka kuwagombanisha tu ndugu hao wa damu.

Lucas naye alivyotoka tu kule polisi alikwenda moja kwa moja nyumbani kwa kaka yake Thomas na kumchukua mwanaye Henry na kuondoka zake kwenda nyumbani kwake kwani alisema kuwa hawezi kumuacha mwanae huyo kwenye nyumba ya muuaji. Lucas pia alifikiria kumpeleka mwanae huyo kesho yake kwa daktari wake ili kuangalia kama kaka yake Thomas alishaanza kumuwekea madawa ya kulevya mtoto wake huyo.

Baada ya kumchukua mwanae Henry kutoka nyumbani kwa kaka yake Thomas, walivyofika nyumbani mwanae huyo alikuwa ni mwenye furaha huku akimuita baba yake na kumwambia baba hivi mara baba vile na Lucas alibaki tu kumuangalia mwanae huyo kwa huruma kwani mtoto wake huyo alikuwa wala hajui chochote kabisa na wala alikuwa hajui kinachoendelea kabisa.

Muda wa chakula ulivyofika Lucas alikula kidogo sana na kwenda chumbani kwake kulala. Akiwa kitandani huku akitafuta usingizi Lucas alianza kuwaza mambo mengi sana kwenye maisha yake mpaka jinsi alivyokutana na mke wake Nancy mpaka walivyopata matatizo na kupelekea mke wake huyo kukamatwa na kushikiliwa na polisi. Alivyowaza jinsi mke wake Nancy alivyokamatwa na yeye alivyomtelekeza na matokeo yake akawa na mwanamke mwingine yaani Stella, Lucas alijilaumu sana kwa kumtelekeza mke wake huyo kipenzi kipindi alichokuwa na matatizo. Alivyowaza hivyo tu Lucas alizidi kushikwa na hasira hasa pale alipokumbuka kuwa ni kaka yake Thomas ndio aliyekuwa akimueleza mara kwa mara kuwa aachane na huyo mke wake Nancy kwa kuwa ni muuaji na atafute tu mwanamke mwingine wa kumuoa wakati kumbe muuaji na aliyekuwa akiyapanga yote hayo ni yeye mwenyewe Thomas ili tu kujipatia mali zake kwa faida zake yeye mwenyewe huku akimuharibia yeye ndoa yake na maisha yake kwa ujumla. Ona sasa yeye na mke wake Nancy jinsi ndoa yao ilivyoyeyuka na kusambaratika kabisa kwani hakutegemea kabisa kama kuna siku itafika mke wake Nancy na ndugu zake watamuona na wala hawatamsalimia kabisa kama ilivyotokea siku hiyo pale polisi wakati walivyoonana na matokeo yake ndugu zake Nancy wakamshika Nancy mkono na kumuongoza kwenye gari bila hata ya kumsalimia yeye.

Lucas alivyowaza hivyo alijisemea moyoni kuwa kweli Nancy ndio mpenzi wake wa kweli kwani mara baada ya kumuona tu siku hiyo pale polisi ameshindwa hata kumfuta mawazoni mwake na bado anamuwaza tu mpaka muda huo na hajui atawezaje kuishi bila yeye hasa baada ya kugundua kuwa yeye hana makosa kabisa na wala sio yeye aliyetaka kumuua. Lucas aliendelea kukumbuka ukarimu, upole, ucheshi na upendo aliokuwa nao mke wake Nancy na roho ilizidi kumuuma sana kwa kuona kuwa amempoteza mke wake huyo kwa urahisi sana.

Pia Lucas aliendelea kuwaza na kujisemea moyoni kuwa ingawa mke wake Nancy amekaa mahabusu kwa miaka 3 na miezi kadhaa na pia isitoshe shuruba zote hizo alizozipitia akiwa huko polisi lakini uzuri wake bado uko dhahiri na bado ni mrembo kama vile hakuwa kwenye matatizo na hakuwahi kupatwa na matatizo yoyote.

Lucas aliendelea kuwaza jinsi yeye alivyokuwa amelazwa hospitali huku mke wake Nancy akimuhudumia na akisaidiwa na kaka yake yeye Lucas yaani Thomas pamoja na mke wake Mary lakini hakujua kumbe muuaji aliyetaka kumuua alikuwa naye hapo hapo huku akijidai kumuhudumia kwa kisingizio tu cha undugu! Kweli jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. Lucas aliwaza sana akiwa kitandani hapo na mwishowe alipitiwa na usingizi.

Kwa kina Nancy nako walikuwa wakifurahia Nancy kuachiwa huru na pia nyumba yao ilikuwa ikijaa wageni kila baada ya muda mfupi hasa majirani zao na baadhi ya ndugu zao waliokuwa wakija ili kuwapa hongera ya Nancy kuachiwa huru na pia kumpa pole Nancy kwa matatizo yaliyomkuta na kumpongeza kwa kuachiwa huru.

Siku hiyo Nancy alikuwa ni kama mtoto mdogo kwa mama yake na baba yake. Pia familia ya Nancy walimuuliza ilikuwaje mpaka akaachiwa huru maana hata wao bado hawaelewi kitu chochote zaidi tu ya baba yake kupigiwa simu kuwa aende kumchukua polisi kwani ameachiwa huru, na pia Lucas aliyekuwa mume wake alikuwa anafanya nini pale polisi!? Je anafahamu kwanini Lucas alikuwepo mahali pale muda ule walivyokuwa wamekwenda kumchukua?

Nancy aliwajibu familia yake na kusema kuwa ukweli yeye hajui chochote kuhusu uwepo wa Lucas mahali pale, isitoshe na yeye ndio alimuona pale pale kama wao tu hivyo hajui chochote.

Pia Nancy aliwaambia familia yake kuwa yeye jana alikuwa amejipumzikia tu huku akijisomea Biblia yake ambayo mama yake alikuwa amempelekea na alivyomaliza kusoma mistari kadhaa akaanza kusali kumuomba Mungu kama siku zote alivyokuwa akisali kuwa siku moja ukweli ujulikane, na alivyomaliza tu kusali na kusema Amen alisikia akiitwa na mmoja wa maaskari waliokuwa wakiwalinda na askari huyo alimwambia kuwa ajiandae kwani kesho anatolewa, na alivyoambiwa hivyo hakuamini kabisa masikio yake na aliona ni kama vile muujiza na asubuhi ndio akatolewa na kuletwa pale kituo cha polisi. Alivyokuwa pale polisi ndio akamuomba yule askari wa kike ambaye walimkuta amesimama naye ampigie simu nyumbani kwao kuwaambia waende kumchukua kwani pale alikuwa hana hata nauli, na bahati nzuri mama yake alikuwa ameandika namba zake za simu na namba za baba yake za simu nyuma ya ile Biblia aliyokuwa amempelekea, hivyo alimpa yule askari namba ya simu ya baba yake, na yule askari alikuwa ni mtu mzuri kweli kwake kwani alivyomuomba tu ampigie simu kwa baba yake alikubali.

Baada ya Nancy kumaliza kuwaambia hivyo, mama yake Nancy alimwambia Nancy kuwa je anayakumbuka maneno yake kipindi kile alichokuwa akimtembelea jela na hasa wakati alivyokuwa akimkuta amekata tamaa? Si anakumbuka mara kwa mara alikuwa akimwambia kuwa Mungu anajibu maombi kwa wakati wake si ameona sasa yeye mwenyewe hatimaye ameachiwa huru! Nancy alimwangalia mama yake na kutabasamu na akasema kuwa ni kweli sasa ameamini kuwa Mungu anajibu maombi ila kinachotakiwa ni kuwa tu mvumilivu kwani huwa anajibu kwa wakati wake anaoona yeye mwenyewe unafaa.

Baada ya Nancy kusema hivyo watu wote waliokuwa hapo kwa kina Nancy walikubaliana na usemi huo na mama yake Nancy alimwambia Nancy kuwa inawezekana pia yeye ameachiwa huru labda itakuwa mapolisi wameshamjua huyo mtu aliyetaka kumuua Lucas na wasubiri tu kwani watajua tu muda si mrefu sababu iliyopelekea maaskari waone kuwa yeye Nancy hana kosa na hivyo kumuachia huru.

Pia mama yake Nancy aliendelea kusema kuwa mpaka sasa hawajasikia fununu yoyote ila wanaanza kuhisi kukamatwa kwa huyo mwanamke aliyekuwa akiishi na Lucas inaweza kuwa ndio sababu tosha ya yeye Nancy kuachiwa huru, labda huyo mwanamke amesema kila kitu ingawa bado wapo gizani kuhusu hili swala.

Baada ya mama yake Nancy kusema hivyo, mara simu ya Julia mdogo wake Nancy iliita na alivyopokea alikuwa ni Rehema ambaye alimwambia Julia kuwa Henry mtoto wa Nancy na Lucas amerudi nyumbani siku hiyo na inaonyesha kuwa amerudi moja kwa moja maana amerudi na vitu vyake karibia vyote lakini hamna jipya mpaka sasa zaidi tu ya Stella kukamatwa na Henry kurudi hapo nyumbani labda kukiwa na jipya atamwambia.

Baada ya Rehema kumwambia hivyo Julia, Julia naye alimwambia Rehema kuwa dada yao Nancy naye ameachiwa huru na kwasasa kesi yake imefutwa. Rehema alifurahi sana kusikia hivyo na alimwambia Julia amefurahi sana hivyo atamwambia na Fatuma pia. Baada ya Julia kumaliza kuongea na Rehema, aliwaeleza watu wote waliokuwa pale kuwa hatimaye Henry amerudi nyumbani kwa baba yake kwani Rehema ndio alikuwa akimwambia hapo kwenye simu. Baada ya Nancy kusikia hivyo moyo wake ulifanya paa maana alijua kuwa mwanae huyo atakuwa ni mkubwa sasa na atakuwa anasoma na kuongea maana alimuacha akiwa na miaka 2 tu wakati alivyokamatwa. Na kwa muda wote huo yeye aliokaa jela sasa hivi atakuwa ni mkubwa sana. Nancy aliendelea kuwaza kuhusu mwanae huyo na aliwaambia wazazi wake na ndugu zake kuwa anatamani sana kumuona mtoto wake huyo hata muda huo lakini wazazi wake na ndugu zake hao walimwambia kuwa asiwe na wasiwasi kwani atamuona tu mwanae kwasababu kwasasa tayari yupo huru hivyo hamna tena kitu cha kumzuia kufanya hivyo na haitakuwa kazi sana kumuona mwanae huyo.

Baada ya wazazi wake na ndugu zake kumwambia hivyo, Nancy aliwaambia kuwa je baba yake yaani Lucas akimkatalia asimuone itakuaje? Wazazi wake na ndugu zake hao walimwambia Nancy kuwa huyo Lucas kwanini amkatalie kumuona mwanae wakati yeye ndio mama mzazi na ndio aliyemleta duniani mtoto huyo!? Mwanzo walikuwa wanamuita yeye muuaji ndio maana walizuia asimuone mtoto wake lakini sasa amkatalie kumwona mwanae kwasababu ipi hasa!? na pia isitoshe hata huyo Lucas atakuwa ametahayari sana sasa baada ya kumuona yeye Nancy akiwa huru na lazima atakuwa na mtihani mkubwa sana tu kwa yote aliyomfanyia. Alidhani yeye Nancy ataozea jela?

Pia ndugu zake Nancy waliendelea kusema kuwa yani hata leo walivyomuona Lucas pale polisi alikuwa akitia huruma sana sijui hata alikwenda kufanya nini pale polisi maana alionekana akiwa amechoka sana, au alijua kuwa Nancy anaachiwa huru siku hiyo ndio maana akaenda labda ili kuhakikisha au?
SEHEMU YA KUMI NA SABA 17

Comments