Sehemu ya - 7
Muda ulienda hatimaye ilipita miaka miwili tangu Nancy ashikiliwe na polisi kwa kuhusika na jaribio la kutaka kumuua mume wake Lucas. Huko mahabusu Nancy alishayazoea maisha ya huko na pia muda wake mwingi alikuwa akiutumia kusali na kumuomba Mungu. Pia Nancy alikubaliana na ukweli kuwa ameshampoteza mume wake Lucas ambaye tangu ashikiliwe na polisi hakuwahi hata siku moja kwenda kumjulia hali wala kumpeleka mtoto wao Henry kumsalimia. Pia Nancy alikubaliana na ukweli kuwa hata ndugu zake Lucas wote walikuwa nao wamemtenga hivyo kwasasa akili yake yote ilikuwa ikimuwaza mtoto wake Henry tu na pia alimshukuru Mungu sana kwa kumpa familia yenye upendo yaani wazazi wake pamoja na wadogo zake Anthony na Julia ambao wamekuwa wakimfariji na kumtia nguvu kwenye hiki kipindi kigumu alichokuwa anakipitia kwasasa.
Wazazi wake Nancy walijitahidi kila walivyoweza ili angalau kumwekea wakili wa kumtetea mtoto wao Nancy na mwishowe waliamua kuuza gari ambalo mtoto wao Nancy aliwanunulia huku akisaidiwa na mume wake Lucas ili kupata pesa za kushughulikia kesi hiyo ya Nancy. Maisha ya wazazi wake Nancy nayo yalizidi kuwa magumu kwani kwa kiasi kikubwa Nancy ndio alikuwa akiwasaidia kuyaendesha maisha yao huku akiwasaidia kuwasomesha wadogo zake Julia na Anthony.
Lucas na ndugu zake walikuwa wakiendelea kufurahia jinsi familia ya Nancy ilivyokuwa ikipata shida na mara kwa mara walikuwa wakisema kuwa mnaona familia ya muuaji inavyoumbuka kwa sasa, huyo muuaji Nancy alitaka utajiri wa haraka ona sasa amekosa kila kila kitu na huo utajiri wala hajaupata na matokeo yake sasa ananyea debe, yani na bado kwani yeye na hao ndugu zake watajiju mpaka wajue kilichomtoa ndege kanga manyoya yake.
Pia mara nyingi ndugu zake Lucas pamoja na Lucas mwenyewe walivyokuwa wakikutana walikuwa wanasema kuwa yani huyo Nancy kutoka uuaji mpaka kuwa mcha Mungu eti sasa hivi ndio wanasikia anajidai kusali na kujifanya mcha Mungu huko mahabusu yani hana lolote anafikiri akijifanya kusali ndio atawarubuni polisi ili wamuachie!
Siku moja wadogo zake Nancy, Julia na Anthony walikwenda kumtembelea dada yao Nancy mahabusu. Nancy alianza kuwaambia wadogo zake hao kuwa anawashukuru sana kwa upendo wanaouonyesha kwake kwani wao pamoja na wazazi wao wamekuwa ni faraja kubwa sana kwake na mpaka sasa imefika miaka miwili tangu yeye apate matatizo hayo lakini hawajamuacha na wala hawakati tamaa na wameendelea kumfariji na kumtia nguvu kila kukicha, ona mpaka sasa ameshazoea maisha hayo ya kuwa mahabusu na wala halii lii tena kama ilivyokuwa mwanzo, yani bila wao labda sasa hivi angekuwa ameshakufa na angekuwa ameshazikwa.
Baada ya Nancy kuwaambia hivyo wadogo zake Julia na Anthony, Julia alimwambia Nancy kuwa asijali kabisa kwani yeye atabaki kuwa ni dada yao hata kama ni kweli alitaka kumuua huyo mume wake Lucas au la lakini kwao yeye atabaki kuwa ni ndugu yao na dada yao wanaompenda sana kwani amewatendea mambo mengi mno mazuri sana tena sana na amewaonyesha upendo wa hali ya juu kwenye maisha yao yote kabla hajapatwa na matatizo, sasa kwanini wao waje wamuache kipindi hichi ambacho yeye ana matatizo na ndio kipindi ambacho anachowahitaji zaidi? Hivyo wao wataendelea kumpa ushirikiano na kumpenda yani no matter what. Pia Julia aliendelea kumwambia Nancy kuwa hata wao wanafurahi sana kumuona sasa akiwa mwenye afya na furaha kidogo sio kama alivyokuwa mwanzo.
Baada ya Julia kumwambia hivyo Nancy, wote kwa pamoja Julia na Anthony waliendelea kumkumbushia Nancy mambo yote mazuri aliyowafanyia akiwa kama dada yao wa kwanza kwa kuzaliwa na hivyo Nancy alibaki tu akitabasamu kwani wakati ule alivyokuwa akiwapenda na kuwaonyesha upendo wadogo zake hao wala hakujua kama anatengeneza mahusiano mazuri nao ambayo yangekuja kumsaidia siku moja, yeye alikuwa akifanya vile kwa upendo tu wa familia yake kwani hakutaka hata siku moja wazazi wake na wadogo zake hao wasumbuke na maisha wakati yeye yupo na ndio maana alikuwa akiwasomesha wadogo zake ili nao waje kupata kazi zao nzuri na wawe na maisha yao mazuri hapo baadaye na familia yao izidi kuwa familia bora na yenye amani na upendo.
Hivyo Baada ya Julia kumwambia hivyo Nancy, Nancy alimwambia Julia na Anthony kuwa anashukuru sana tena sana kwasababu hawajamuacha kwenye kipindi hiki kigumu kinachomkabili. Pia Baada ya Nancy kusema hivyo, aliwaangalia wadogo zake hao na aliwauliza je mtoto wake Henry anaendeleaje? Na je mume wake Lucas naye anaendeleaje?
Baada ya Nancy kuwauliza hivyo wadogo zake hao, mdogo wake Julia alimwambia Nancy kuwa kusema ukweli kuna mambo mengi sana yanaendelea huko kwa mume wake Lucas sema tu wazazi wao huwa wanawakataza wasimwambie yeye Nancy kitu chochote. Baada ya Julia kusema hivyo Nancy huku akionyesha kuwa ni mwenye shauku aliwaangalia wadogo zake hao wote wawili na kuwauliza kuwa je ni mambo gani hayo!? Wakati Julia anataka kuanza kumweleza Nancy, Anthony alimuita ndugu yake Julia kwa nguvu na kusema ?Julia!!?
Baada ya Anthony kumuita Julia kwa nguvu, Julia alimgeukia Anthony na kumwambia Julia nini!? Sasa watamficha dada yao huyo mpaka lini!? si bora tu wamueleze ukweli wote wa mambo yanayoendelea huko uraiani hasa kwa huyo mume wake Lucas labda inaweza kumsaidia akawa na amani moyoni mwake, maana siku zote kama kuna kitu kinaendelea na mtu hajaambiwa amefichwa lazima huyo mtu anakuwa kwenye wasiwasi mkubwa mpaka pale atakapoambiwa ukweli, hivyo watamtesa dada yao huyo mpaka lini!? Si bora tu amwambie ukweli.
Baada ya Julia kumjibu hivyo Anthony, Anthony alimwambia Julia kuwa shauri yake kwa hicho anachokifanya kwani wazazi wao sio wajinga kuwakataza wasimwambie kitu chochote dada yao Nancy hivyo yeye hayumo kwa lolote litakalotokea.
Nancy alikuwa yupo kimya huku akiwasikiliza wadogo zake hao na mazungumzo yao ndio yalizidi kuanza kumchanganya na hivyo kwa haraka haraka alianza kufikiria mambo mengi na mwishowe aliwaza na kujisemea kuwa au mtoto wake Henry amepatwa na tatizo lolote au amekufa!? Labda ndio maana mume wake Lucas anaogopa kuja kumtembelea ili kumkwepa kwani anajua akienda hapo atamuuliza kuhusu mwanae huyo!? Na hivyo baada ya kuwaza hivyo Nancy alimwambia mdogo wake Julia kuwa anaomba tu amwambie ukweli kwani huko kwa mume wake Lucas kuna nini!? Au mtoto wake Henry amepatwa na tatizo lolote?
Julia alimwambia dada yake Nancy kuwa atamueleza tu ukweli wote ila kwanza amuahidi kuwa hata panic kwa kile atakachomueleza.-
Baada ya Julia kumwambia dada yake Nancy kuwa atamueleza tu ukweli wote ila kwanza amuahidi kuwa hata panic kwa kile atakachomueleza, Nancy alimuhakikishia mdogo wake Julia kuwa wala hata panic hivyo amueleze tu ukweli na wala asimfiche kitu chochote kwani kwasasa alivyo sio kama zamani, na pia sasa hivi anaweza kuchukua kitu chochote kwenye moyo wake hata kiwe kibaya na kizito kiasi gani.
Baada ya Nancy kumwambia hivyo Julia, Julia alianza kumwambia Nancy kuwa wala asiwe na wasiwasi wowote kwani mwanae Henry ni mzima wa afya lakini ukweli ni kwamba hawajamuona mtoto wake huyo wala kumtia machoni hata kwa mbali sasa yapata kuwa ni mwaka mmoja na miezi kama kumi hivi.
Baada ya Julia kumwambia hivyo Nancy, Nancy alishtuka kidogo na alimuuliza Julia kuwa sasa kama hawajamuona mtoto wake Henry kwa muda wote huo wanajuaje kama ni mzima na pia kwanini hawajamuona!? Yani kweli wanashindwa kwenda nyumbani kwa mume wake Lucas ili kumuona mtoto wake!?
Baada ya Nancy kusema hivyo, Julia alimwambia dada yake huyo kuwa atulie mbona sasa ameanza ku panic wakati ndio kwanza anaanza kumuelezea basi kama ni hivyo ataacha kumwambia. Nancy alimwambia mdogo wake Julia kuwa basi hata panic tena hivyo aendelee tu kumuelezea, wakati Nancy akimwambia hivyo Julia bado alikuwa na shauku kubwa sana ya kutaka kufahamu kwanini ndugu zake hao na wazazi wake hawajamuona mtoto wake huyo kwa muda wote huo halafu wanabaki tu kumdanganya kila siku kuwa mwanae huyo hajambo na anaendelea vizuri, maaana kama hawajamuona kwa muda wote huo wanajuaje kama anaendelea vizuri!?
Baada ya Nancy kumuomba mdogo wake Julia aendelee tu kumwambia kwani hata panic Julia aliendelea kumwambia Nancy kuwa sababu kubwa iliyowafanya wasimuone mtoto wake Henry ni kuwa mume wake Lucas aliwafukuza yeye na Anthony ambapo walikuwa wanakaa ili kumsaidia kumlea Henry na pia kumpa kampani wakati yeye Nancy akiwa hayupo na mwanzoni shemeji yao huyo alikuwa akifurahia uwepo wao kwani mara nyingi alikuwa akienda sehemu mbalimbali na Anthony na pia walikuwa wakiangalia mpira na Anthony na mambo mengine kibao lakini ghafla alianza kuwabadilikia na siku moja aliwafukuza kabisa yeye Julia na Anthony kutoka hapo nyumbani kwake na kibaya zaidi wakati anawafukuza aliwatamkia kabisa kuwa waondoke hapo nyumbani kwake kwani yeye hawezi kufuga familia ya wauaji na kibaya zaidi alisema kuwa eti yeye Nancy alitaka kumuua yeye mwenyewe bora hata angeamua kumuua mtu mwingine na pia kwa taarifa yao atahakikisha yeye Nancy anaozea jela.
Baada ya Julia kusema hivyo Nancy huku akiwa ni mwenye huzuni alisema kuwa ingawa walikuwa wakimficha na hata alivyojaribu kumuuliza mama yao kuhusu mume wake Lucas na ndugu zake kutokwenda kumuangalia mama yao huyo naye alikuwa akimwambia kuwa eti asiwe na wasiwasi kwani Lucas bado anahitaji mapumziko baada ya mambo yaliyomtokea lakini wakati mama yao akimwambia hivyo yeye tayari alishajua kuwa mume wake huyo ameamua kuwa naye mbali na pia hata ndugu wa mume wake nao wameamua kumtenga hivyo anachomueleza leo wala hashangai kabisa kwani alilijua hilo kuwa lipo na kama halipo basi linakuja.
Baada ya Nancy kusema hivyo, Julia alimwambia Nancy kuwa amefurahi sana kuona kuwa wala hajapanic na pia amechukulia kawaida tu sasa walivyokuwa hawataki kumwambia ukweli sijui walikuwa wanaogopa nini, hivyo leo yeye atamueleza kila kitu na hatamficha kitu chochote.
Baada ya Julia kumwambia hivyo Nancy aliendelea kumwambia dada yake huyo kuwa hivyo tangu siku hiyo yeye na Anthony waliyofukuzwa na shemeji yao Lucas hawajaonana nae tena na pia Lucas alimpeleka mtoto wao Henry kwa kaka yake Thomas na hata wazazi wao walivyojaribu kwenda kumuomba basi wamlee wao Henry, Lucas alikataa katakata na tangu wakati huo amekuwa akiwakwepa na hata ikitokea wamemuona huko mabarabarani amekuwa akipandisha kioo kabisa kama alikuwa ameacha kioo wazi na pia amekuwa akiendesha kwa spidi kali huku akiwatimulia vumbi bila hata ya kuwasalimia na amekuwa akiwafanyia hivyo wao wote yani hata wazazi wao baba na mama yao.
Pia Julia aliendelea kumwambia Nancy kuwa yani ili kufahamu Henry anaendeleaje yeye amekuwa akiwasiliana na wasichana wao wa kazi Rehema na Fatuma na wao ndio wamekuwa wakimueleza karibia kila kitu kinachoendelea hapo nyumbani kwa huyo mume wake Lucas.
Baada ya Julia kusema hivyo, Nancy aliendelea kusikitika na alimwambia Julia kuwa yani alivyomtajia Rehema na Fatuma ndio amemkumbusha mbali zaidi yani hata wao hawamkumbuki kweli! hata kuja kumuangalia tangu alivyokamatwa!? Yani wema wote ule aliowatendea lakini sasa hivi inaonyesha wamesahau kila kitu! Kwani tangu aanze kuishi nao miezi kadhaa tu baada ya yeye kuolewa na Lucas ameishi nao vizuri sana na aliwapenda kama wadogo zake na aliwafanya wajisikie kama ni ndugu zake na si wasichana wa kazi lakini leo wema wote aliowafanyia ndio wanachomlipa hicho!? Lazima tu na wao watakuwa wanamuona kuwa yeye ni muuaji na hafai tena ndio maana hata hawajisumbui kwenda kumsalimia na kumjulia hali yake.
Baada ya Nancy kusema hivyo Julia alimwambia Nancy kuwa akiwalaumu Rehema na Fatuma atakuwa anakosea kabisa kwani akumbuke kuwa wale ni wafanyakazi tu pale nyumbani kwa Lucas na hivyo wanamsikiliza bosi wao Lucas lakini kiukweli hata wao wanaumia sana kwa matatizo yaliyompata na mambo yote anayopitia kwasasa ila sema hawana jinsi na kibaya zaidi Lucas alishawakataza kwenda hapo mahabusu kumuona na ameshawaambia kabisa kuwa mtu atakayethubutu kwenda kumuona yeye Nancy huko mahabusu basi siku hiyo anavyoenda huko mahabusu abebe na begi lake kabisa kwani akitoka huko mahabusu inabidi apitilizie kwenye kituo cha basi ili kurudi kijijini kwao sasa hata kama angekuwa yeye Nancy unafikiri angefanyaje?
Julia aliendelea kumwambia Nancy kuwa na akumbuke kuwa kazi yao wanaipenda kwani ndio inayowawezesha kusaidia familia zao huko kijijini na mpaka wanasomesha wadogo zao kwa huo huo mshahara wanaoupata sasa wakifukuzwa kazi wataishije!?
Julia aliendelea kumwambia Nancy kuwa kuna siku walijiandaa kabisa kwenda hapo mahabusu kumuona sasa wakiwa wanamsubiri yeye Julia ili aende akawapitie ndio Lucas akawakuta wakiwa wamebeba na vikapu vya chakula na alivyowauliza wanakwenda wapi ndio wakamwambia kuwa wanataka kwenda mahabusu kumuona yeye Nancy yani bado nusu tu awafukuze kazi siku hiyo hivyo ilibidi wamuombe sana msamaha huku wakilia na walimwambia kuwa hawatarudia tena na yeye ndio akawaambia kuwa marufuku kwenda huko mahabusu na pia aliwaambia kuwa kuanzia siku ile wasiwakaribishe ndugu wa aina yeyote wa kwake yeye Nancy yani hata wao Anthony na Julia na hata wazazi wao ndio maana tangu siku hiyo Rehema na Fatuma hawajajaribu tena kuja kumuona na pia ingawa hawaendi kumuona lakini huwa wanaongeaga naye yeye Julia kisirisiri kumuulizia yeye Nancy anavyoendelea na pia huwa wanamueleza yeye Julia mambo yote yanayoendelea hapo nyumbani kwa Lucas.
Baada ya Julia kumwambia hivyo Nancy, Nancy alizidi kuumia lakini alijikaza ili mdogo wake Julia asimgundue na matokeo yake akaacha kumuhadithia yanayoendelea huko nyumbani kwa mume wake Lucas, hivyo wakati Nancy akihuzunika Julia alimwambia Nancy kwa upole kuwa na pia kwasasa mume wake huyo anaishi na mwanamke mwingine.
Baada ya Julia kumwambia hivyo Nancy, Nancy alishtuka na kujiona kama vile anaota na alimuuliza Julia kuwa eti amesemaje!? Wakati Nancy akimuuliza hivyo Julia, Anthony ambaye muda wote alikuwa yupo kimya akimsikiliza Julia anavyomuhadithia dada yao Nancy mambo yanayoendelea huko kwa mume wake Lucas, alimwambia tena Julia kwa ukali kuwa ?wewe Julia unafanya nini sasa! Yani mambo yote hayo uliyomwambia unaona hayatoshi mpaka umwambie na hayo mengine ambayo hata hayakuhusu?!
Baada ya Julia kumwambia Nancy kuwa kwasasa mume wake Lucas anaishi na mwanamke mwingine na Anthony kumwambia Julia kwa ukali kuwa anafanya nini sasa! Yani mambo yote hayo aliyomwambia dada yao Nancy anaona hayatoshi mpaka amwambie na hayo mengine ambayo hata hayamuhusu, Julia alimjibu Anthony na kumwambia kuwa Nancy ni dada yao na mambo yake pia yanawahausu hata wao, kwani hata yeye Anthony hajaumia mambo anayoyafanya huyo shemeji yao Lucas!? Hivyo leo atamueleza dada yao huyo kila kitu na anajua ataumia sana lakini kadri siku zitakavyozidi kwenda atasahau na yatapita tu na uchungu wote utamuisha kuliko wanavyomficha kila kitu mpaka vitu muhimu vya maisha yake na familia yake.
Baada ya Julia kumwambia hivyo Anthony, Nancy naye ingawa bado alikuwa ana uchungu na alitamani sana kusikia mengi kutoka kwa mdogo wake Julia alimwambia mdogo wake Anthony kwa upole kabisa kuwa asiwe na wasiwasi kwani ni kweli mambo anayomueleza Julia yanamuumiza sana tena sana lakini ni bora akajua tu ukweli na ataumia kwa muda lakini itafika wakati atasahau kuliko wanavyomficha kwani wanavyomficha amekuwa ni mtu mwenye mawazo mengi sana kichwani mwake na mara nyingi sana amekuwa akijiuliza maswali mengi sana ambayo hayana majibu na matokeo yake mawazo hayo yamekuwa yakimuumiza sana na ndio kwa kiasi fulani huwa yanachangia sana kudhoofisha afya yake. Ona kwa jinsi walivyokuwa wakimficha kuna wakati mpaka alikuwa akiwaza labda sababu inayofanya mume wake Lucas asije kumuona na kumjulia hali labda alishakufa kwa madhara aliyoyapata ya kupigwa na ile risasi. Sasa wakati wakimdanganya kuwa mume wake anashindwa kwenda kumuona kwasababu bado anapumzika, na wakati yeye anasikitika na kumuwaza mume wake huyo atakuwa amepatwa na tatizo gani au labda amekufa kumbe mwenzake huyo ni mzima wa afya na ameshamsahau yeye kabisa tena kwa kipindi kifupi na tayari anaishi na mwanamke mwingine! Yani hakutegemea kabisa! yani katika mambo yote ambayo hakutegemea kufanyiwa na Lucas basi hilo la Lucas kuamua kuishi na mwanamke mwingine - wakati yeye Nancy akiwa bado yuko hai hakulitegemea kabisa kwenye maisha yake. Na baada ya Nancy kusema hivyo huku akilengwa lengwa na machozi alimwambia mdogo wake Julia kuwa aendelee kumweleza kila kitu na asimfiche kitu chochote maana angalau amejua kinachoendelea huko na angalau leo amejua kuwa mtoto wake Henry ni mzima wa afya na hana matatizo yoyote kama alivyokuwa akifikiria mwanzo na pia amejua kuwa mume wake Lucas naye hana matatizo yoyote kama alivyokuwa akifikiria na pia ni mzima wa afya sema tu ameamua kumsahau kabisa yeye na kumtoa kabisa kwenye mawazo na maisha yake.
Baada ya Nancy kumwambia mdogo wake Julia kuwa aendelee kumweleza kila kitu na asimfiche kitu chochote maana angalau amejua kinachoendelea huko nyumbani kwa mume wake na angalau leo amejua kuwa mtoto wake Henry ni mzima wa afya na hana matatizo yoyote kama alivyokuwa akifikiria mwanzo na pia amejua kuwa mume wake Lucas naye hana matatizo yoyote kama alivyokuwa akifikiria na pia ni mzima wa afya sema tu ameamua kumsahau kabisa yeye na kumtoa kwenye mawazo na maisha yake, Julia aliendelea kumwambia dada yake Nancy kuwa kama alivyokuwa amemueleza mwanzo ni kwamba mume wake Lucas kwasasa anaishi na mwanamke mwingine, na hata kabla Julia hajaendelea kusema alichokuwa akitaka kusema Nancy alimuuliza Julia kuwa lakini amesema kuwa kwasasa hawaonani kabisa na mume wake huyo na wala nyumbani kwake hawaendi tangu mume wake huyo awafukuze sasa je amejuaje kama mume wake ana mwanamke mwingine!? Julia alimwambia dada yake huyo kuwa mbona sio siri tena kwani kila mtu anajua sasa kuwa Lucas ana mwanamke mwingine na anaishi naye nyumbani kwake, yeye mwanzo aliambiwa na wasichana wa kazi wa Lucas yaani Rehema na Fatuma maana wanawasiliana sana kwenye simu lakini hakutilia maanani sana mpaka siku moja alivyowaona Lucas na huyo mwanamke yeye mwenyewe kwa macho yake kwenye gari kwani siku hiyo aliyowaona yeye alikuwa amesimama kwenye kituo cha mabasi akisubri basi sasa hana uhakika kama shemeji yake huyo hakumuona ndio maana alimpita au alimuona lakini alifanya makusudi kama vile hajamuona na kumpita.
Baada ya Julia kumwambia hivyo dada yake Nancy, Nancy alishusha pumzi kwa nguvu na kusema kweli anaona Mungu ameamua kumuacha kabisa yani yeye anavyozidi kusali na mateso ndio yanavyozidi kumfikia sijui alikosa nini!
Julia aliendelea kumwambia Nancy kuwa kwa jinsi wasichana wa kazi wa Lucas yaani Fatuma na Rehema walivyomuelezea ni kuwa huyo mwanamke alianza kufika pale nyumbani kwao kama miezi 6 hivi iliyopita yaani ikiwa imepita mwaka mmoja na miezi sita tu tangu yeye Nancy akamatwe na polisi na kuwekwa mahabusu. Hivyo huyo mwanamke alikuwa anaenda kutembea na kuondoka na mwishowe akawa anaenda siku za ijumaa na kulala mpaka jumatatu ndio akawa anaondoka na sasa hivi ndio amehamia kabisa yaani anakaa hapo hapo nyumbani kwa Lucas na kwa jinsi Rehema na Fatuma walivyomueleza ni kuwa huyo mwanamke amehamia nyumbani hapo rasmi kama miezi 3 hivi na wiki kadhaa zilizopita.
Pia Julia alimwambia Nancy kuwa si anakumbuka kuwa yeye Nancy aliwahi kumwambia yeye Julia na mama yao kuwa mume wake Lucas amemuagizia gari jipya kabisa na la gharama kubwa kutoka Japan? Nancy alimjibu Julia na kumwambia ndio anakumbuka aliwahi kuwaambia kuhusu hilo, na kweli bora amemkumbusha maana hata mambo ya hilo gari alikuwa ameshayasahau kabisa je hilo gari lilishafika? Julia alimwambia Nancy kuwa ndio hilo gari lilifika miezi 3 tu tangu yeye Nancy akamatwe na kushikiliwa na polisi, na tangu lilivyofika hilo gari mume wake Lucas alikuwa amelipaki tu na wala hakuwahi kuliendesha lakini sasa ndio anaendesha huyo mwanamke wake inavyoonyesha ndio amempa yeye kwani kwa jinsi kina Rehema na Fatuma walivyomwambia ni kwamba siku moja Lucas na huyo mwanamke walishinda sebuleni hapo nyumbani wenyewe wakiwa na furaha huku wakinywa vinywaji na kula nyama walizokuwa wamewaagiza kina Fatuma na Rehema wawatengenezee halafu kwenye mida ya jioni waliona Lucas anatoka nje huku amemshika mkono huyo mwanamke na wao walivyochungulia kutoka dirishani waliona Lucas akimuonyesha ufunguo wa gari huyo mwanamke na huyo mwanamke alianza kufurahia na wakakumbatiana kwa furaha halafu huyo mwanamke akaingia kwenye hiyo gari na kuiwasha. Huyo mwanamke alivyomaliza kuiwasha hiyo gari alishuka kutoka kwenye hiyo gari na wote wawili wakiwa na furaha walirudi tena sebuleni na wakaendelea na furaha yao. Hivyo kina Rehema na Fatuma walivyomwambia yeye Julia kuwa Lucas amempa huyo mwanamke wake mpya gari lake jipya ambalo amelinunua wakati yeye Nancy akiwa tayari ameshakamatwa yeye Julia moja kwa moja alijua tu lazima hilo gari walilomwambia kina Rehema na Fatuma ya kwamba Lucas amempa mwanamke wake litakuwa ndio hilo hilo gari ambalo yeye Nancy alikuwa amemwambia yeye Julia na mama yao kuwa Lucas amemuagizia kutoka Japan, maana kwa maelezo ya kina Rehema na Fatuma -ni kwamba hilo gari Lucas alilompa huyo mwanamke ni zuri sana na tena ni la gharama sana. Baada ya Julia kumwambia hivyo Nancy, Nancy alianza kulia na aliona kama vile amebanwa na tumbo la kuharisha na hivyo alishikilia tumbo lake na kumwambia Julia kuwa basi anaomba asiendelee kumwambia tena mambo mengine kuhusu mume wake Lucas na huyo mwanamke wake maana anaona kadri anavyozidi kumwambia hata uvumilivu umeanza kumshinda sasa.
SEHEMU YA NANE 8

Comments
Post a Comment