Koffi Olomide apagawisha wakazi wa Dar

Mzee wa selfee akicheza pamoja na wanenguaji wake.
Muimbaji wa Koffi Olomide, Cindy akifanya yake.
…Akipiga Selfee na baadhi ya mashabiki zake walioweza kucheza vizuri staili ya wimbo huo.
Muimbaji wa Muziki wa Dansi Bongo, Christian Bella, akitumbuiza jukwaani.
Msanii wa filamu Bongo, Jacob Steven ‘JB’, akisakata muziki.
Baadhi ya mashabiki waliohudhuria kwenye shoo hiyo. MWANAMUZIKI kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Koffi Olomide, usiku wa kuamkia leo aliwapagawisha vilivyo mashabiki wake waliohudhuria katika onesho lake liitwalo ‘16 Selfie’ lililofanyika ndani ya Ukumbi wa Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam. Katika shoo hiyo iliyokuwa na mashabiki wengi ilitawaliwa na shangwe kutoka kwa wapenzi wa muziki wa Dansi ambao walijitokeza mapema kwa ajili ya kumshuhudia nguli wa muziki huo akifanya makamuzi yake ya kwanza jijini Dar siku chache tu baada ya kuachia albam yake mpya ya Selfie. Shoo hiyo ilisindikizwa na baadhi ya wanamuziki wa hapa nchini akiwemo Christian Bella na Ruby. (Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)

Comments