Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
Stori: Mayasa Mariwata na Brighton Masalu
MKALI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameifuta aibu ya familia iliyokuwa ikiwakabili kwa kuamua kuifanyia ukarabati nyumba aliyozaliwa na kukulia, iliyopo maeneo ya Tandale-Uzuri jijini Dar Risasi linaripoti.

Nyumba ya akina Diamond iliyopo maeneo ya Tandale-Uzuri jijini Dar.
Novemba 2, mwaka huu, gazeti la Ijumaa Wikienda liliripoti habari ilionesha kuwa nyumba hiyo ambayo anaishi mama’ke mdogo Diamond na ndugu wengine, inamtia aibu yeye na familia nzima kwani choo chake kimeharibika na kimejaa hivyo kuleta usumbufu kwa majirani.
Mtoa ‘ubuyu’ mmoja wa kujitegemea aliwaambia waandishi wetu kuwa baada ya gazeti hilo kuripoti habari hiyo, Diamond alijisikia vibaya akaamua kumpa jukumu la ujenzi mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’ aende kusimamia ujenzi huo.
“Njoeni Tandale mtamkuta mama D (mama Diamond) yupo bize kwelikweli kusimamia ujenzi wa nyumba ile iliyokuwa inatia aibu, ameongeza kozi mbili juu, anaweka paa la Mzauz, yani ikikamilika itakuwa bomba balaa,” alisema mtoa ubuyu huyo.
Baada ya waandishi wetu kufika eneo hilo, mama Diamond alipoulizwa kuhusu ujenzi huo, alifunguka:
“Mnataka kusema nini? Maana Nasibu (Diamond) ameamua kukumbuka kwao kwa kukarabati, amezaliwa na kukulia hapa, hii ni nyumba ya bibi yake, na chumba alichokuwa akiishi Diamond kipindi hicho ni hiki,” alisema mama Diamond huku akiwaelekeza waandishi wetu kwa ufasaha chumba hicho.

Comments
Post a Comment